Ureno wacharazwa na Cape Verde

Odair Fortes 

Ureno walihangaishwa na wanyonge Cape Verde kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Jumanne, vijana hao wa visiwa hivyo vya Afrika wakiwalaza 2-0.

Ureno, ambao hawakutumia hata mchezaji mmoja kutoka kwa waliolaza Serbia mechi ya kfuuzu kwa Euro 2016 Jumapili waliumbuliwa na mabao mawili ya kipindi cha kwanza ambayo yalifungwa katika kipindi cha dakika sita.

Masaibu ya Ureno yalizidishwa na kufukuzwa uwanjani wa Andre Pinto kipindi cha pili.

Odair Fortes alifungua ukurasa wa mabao upande wa Cape Verde dakika ya 37 kwa ustadi mkubwa baada ya krosi yake kutoka kulia kuonekana kushika kasi angani na kumbwaga kipa wa Ureno Anthony Lopes.
Mkabaji wa kati Gege alifunga la pili kwa kufunga kwa stadi kutoka mlingoti wa mbali kufuatia frikiki iliyochapwa na nahodha wa Cape Verde Heldon ambayo ilihepa miguu mingi kabla ya kumfikia.


Mechi hiyo, ambayo ilikuwa ya kusaidia waathiriwa wa mlipuko wa volkano kisiwa cha Cape Verde cha Fogo Novemba mwaka jana, iligeuka masaibu zaidi kwa Ureno Pinto alipoonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo Heldon.

Mabadiliko mengi kipindi cha pili yaliyofanywa na timu zote mbili yalivuruga mtiririko wa mechi, lakini vijana hao wa Afrika walihimili vishindo na kwa urahisi wakaondoka na ushindi huo wa kihistoria.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA