PLUIJM AKIRI YANGA KUBANWA NA STAND UTD
Licha ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 juzi, kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema kuwa wapinzani wao Stand United kutoka Shinyanga waliwazidi uwezo katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wageni Stand ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lao la Yanga lakini baadaye wenyeji walisawazisha na kuongeza la pili lililodumu hadi mapumziko. Stand walisawazisha mapema kipindi cha pili, kabla ya Yanga kupata penalti iliyowapa ushindi wa 3-2 katika dakika za lalasalama.
Akizungumza juzi baada ya mechi hiyo, Pluijm alisema kwamba kikosi chake hakikucheza vizuri, wachezaji hawakuwa na maelewano katika mchezo huo licha ya kushinda.
Alisema kuwa pengo la mabeki, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kelvin Yondani, lilionekana wazi katika mechi hiyo ambayo Stand United ilionyesha soka la kiwango cha juu licha ya kuwa ugenini.
"Timu ilifanya makosa kadhaa, kulikuwa hakuna mawasiliano kati ya Twite (Mbuyu) na Rajab (Zahir), hawakuweza kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara yaliyokuwa yanakuja kwenye lango letu, kwa kifupi hatukucheza vizuri," alisema Pluijm, raia wa Uholanzi.
Aliongeza kwamba amepona mapungufu hayo na kuahidi kuyafanyia kazi na kuwaweka wachezaji wote kuwa tayari kuziba mapengo ya wenzao pale watakapohitajika.
Naye kocha wa Stand United Mganda, Martin Lule, alisema kwamba timu yake imepoteza mchezo huo kwa bahati mbaya lakini vijana wake walionyesha soka la kuvutia.
Mganda huyo alisema kwamba Yanga ni timu ya kawaida na kiwango chake si cha kuhofia hivyo anaahidi msimu ujao atahakikisha hapotezi tena dhidi ya vinara hao wa ligi kuu.
"Yanga inawachezaji wa kawaida, tumefungwa kama mechi nyingine tunavyofungwa, haina wachezaji tofauti na timu nyingine, wana viwango vya kawaida," aliongeza kocha huyo.
Baada ya ushindi huo wa juzi, Yanga ilifikisha pointi 49 na hivyo kuhitaji pointi sita tu ili kutangazwa mabingwa wapya wa ligi wakati Stand United yenye pointi 28 iko katika nafasi ya nane kwenye msimamo.