MALINZI AKIRI KUVURUNDA

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema panguapangua ya ovyo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu imelichafua shirikisho hilo la soka nchini, hivyo wanajipanga kuhakikisha fedheha hiyo haijirudii.

Malinzi, kiongozi wa zamani wa Yanga, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi kuwa mara tu baada ya kumalizika kwa msimu huu wa VPL Mei 9, mwaka huu, vyombo vya TFF vitakutana na kupanga ratiba makini ya msimu ujao.

"Ratiba ya VPL msimu huu imetia doa. Tulifanya makosa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ratiba yetu haikujali michuano hiyo. Msimu ujao tutahakikisha tunakuja na ratiba itakayojali matukio yote ya soka yakiwamo mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ratiba ya Taifa Stars na Taifa Stars Maboresho maana programu ya maboresho ni ya kudumu," alisema Malinzi.


TFF imefanya marekebisho makubwa ya ratiba ya VPL msimu huu mara tatu. Ligi hiyo ilipaswa kuanza Agosti 24, mwaka jana lakini ikapanguliwa hadi Septemba 20 kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi hata hivyo.

Mabadiliko ya pili yalifanywa mwanzoni mwa Oktoba mechi za raundi ya nne zilizokuwa zichezwe Oktoba 12 zikapigwa kalenda hadi Oktoba 18 kupisha mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyokuwa kwenye kalenda ya FIFA ya Taifa Stars dhidi ya Benin.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA