Gervinho kukaa nje wiki tatu

Gervinho 

Straika matata wa Roma Gervinho atakaa nje wiki tatu baada ya kuumia misuli ya paja, hilo likiwa pigo kuu kwa matumaini ya klabu hiyo ya Serie A kumaliza nambari mbili msimu huu.

Taarifa kutoka kwa klabu hiyo ilisema: "Gervinho alichunguzwa mara kadha na imebainika ana jeraha la ngazi ya kwanza paja lake la kulia. Kuna uwezekano atakaa nje wiki tatu.

“Kuanzia kesho ataanza kuponya jeraha.”
Gervinho, ambayea meshindwa kufungia vijana hao wa Rudi Garcia ligini tangu Novemba, atakosa mechi zijazo za ligi dhidi ya Napoli, Torino, Atalanta nap engine Inter Milan Aprili 25.

Roma wamo nambari mbili Serie A, alama 14 nyuma ya viongozi Juventus lakini alama moja pekee dhdii ya wapinzani wao wa jiji Lazio kukiwa na mechi 10 zilizosalia msimu huu.


Kutokuwepo kwa Gervinho kuna maana kwamba Garcia, ambaye timu yake sasa ni kama imepoteza matumaini ya kupigania taji baada ya kutoka sare mechi nane kati ya tisa walizocheza majuzi, huenda akampa presha zaidi sasa mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Seydou Doumbia.

Doumbia alijiunga na klabu hiyo Januari kutoka CSKA Moscow lakini ameshindwa kutamba uwanjani Stadio Olimpico kufikia sasa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA