REAL MADRID YAENDELEZA REKODI YAKE YA USHINDI

Karim Benzema

Cristiano Ronaldo alifunga mawili na kusaidia viongozi wa La Liga Real Madrid kutwanga Almeria 4-1 na kuongeza mkimbio wao wa kushinda hadi mechi 20 Ijumaa.

Ronaldo alifunga dakika 10 za mwisho na kufikisha idadi ya mabao aliyofunga ligini hadi 25 alipofikia mpira wa Karim Benzema uliokuwa umezimwa na kisha akafunga kutoka kwa pasi ya Isco kutoka katikati ya eneo la hatari na kukamilisha ushindi huo.

Real wanaongoza jedwali la ligi na alama 39 kutoka kwa mechi 15, alama tano mbele ya Barcelona watakaotembelea Getafe Jumamosi.

Kiungo wa kati Isco alikuwa ameweka Real kifua mbele kwa kombora kali la kujipinda kutoka nje ya eneo la hatari dakika ya 15 kabla ya Almeria kusawazisha kwa kombora la mbali lililotoka kwa Verza.

Gareth Bale kisha alifunga kwa kichwa kutokana na krosi ya Toni Kroos na kuweka Real 2-1 mbele wakati wa mapumziko.


Kipa Iker Casillas baadaye aliweka wageni mbele kwa kukomboa penalti ya Verza katikati ya kipindi cha pili kabla ya Ronaldo kufunga mabao yake mawili.

Real watasafiri Morocco wiki ijayo kwa Kombe la Dunia la Klabu wakiwa na mechi mbili zaidi walizoshinda ikilinganishwa na mkimbio bora zaidi wa awali wa klabu ya Uhispania uliowekwa na Barcelona wa mechi 18 kuanzia Oktoba 2005 hadi Januari 2006.

Almeria, waliomfuta kocha wao Francisco Rodriguez Jumanne iliyopita na wakammteua Juan Ignacio Martinez kuwa mrithi wake kufuatia mechi hiyo ya Real, wamo eneo la kushushwa ngazi wakiwa na alama 10.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA