KAZI KWAMAGIWJI CHELSEA, LIVERPOOL.



Vinara wa ligi ya Premier ya Uingereza Chelsea na miamba wenzao Liverpool waliotatizika watakuwa miongoni mwa vilabu vitakavyo wania kukaribia Wembley kwenye robo fainali za Kombe la Ligi wiki hii.
Chelsea watatembelea Derby County wanaocheza daraja la kwanza Jumanne huku Liverpool wakichuana na vingozi wapya wa ngazi hiyo, Bournemouth Jumatano.
Kwenye kivumbi cha timu za Premier, Tottenham Hotspurs watatoana jasho na Newcastle United huku Sheffield United wa daraja la tatu watachuana na Southampton ambao wamekosa mwelekeo.

“Timu hii ina ahadi kubwa na mambo yameenda vyema musimu huu lakini hatujashinda lolote kwa sasa na hakuna haja ya kulinganisha kikosi cha sasa na vile vilivyotangulia hadi mwisho wa musimu,” golikipa Petr Cech alisema.


Mlinda lango huyo aliyecheza kwenye ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Hull City mwishoni mwa juma baada ya Thibaut Courtois kuumia anatarajiwa kuanza Jumanne.

Kocha msaidizi wa Bournemouth, Jason Tindall ameeleza shirika la habari la BBC kuwa wananuia kuongezea Liverpool machungu baada ya vijana wa Brendan Rodgers kucharazwa magoli tatu bila jibu kwenye ugenini mwa watanashari wao Manchester United Jumapili.
“Kila mmoja hapa anatia bidii za ziada na tunafurahia kupata mazao,” Tindall aliongeza.

Ratiba
Jumanne (majira ya 1945GMT)
Derby County v Chelsea, Sheffield United v Southampton
Jumatano
Bournemouth v Liverpool, Tottenham Hotspur v Newcastle United

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA