HAKUNA MAKOSA KUMWACHIA LAMPARD- MOURINHO

Frank Lampard 

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho hajuti kumwachilia kiungo nyota mkongwe Frank Lampard kuondoka licha ya kubobea kwake akichezea mabingwa wa ligi ya Premier Manchester City.

Vingozi Chelsea na City wanashindania vikali taji hilo wakitenganishwa na alama tatu pekee huku Manchester United wakiwa point inane nyuma ya vinara katika nafasi ya tatu.

Lampard, 36, aliondoka Chelsea Juni baada ya miaka 11 ya ufanisi kama kiungo kigezo cha kati ambapo alivunja rekodi ya mabao ya klabu hicho na kujiunga na timu ya Marekani, New York City.

Klabu hicho kilimwazima kwa mkopo kwa wamiliki wao Manchester City na amewafungia magoli sita ikiwemo bao la kipekee na la ushindi Jumamosi dhidi ya wavuta mkia Leicester City.


“Maoni yangu ni ikiwa unataka kutizama mbele, watu kama (Cesc) Fabregas, (Nemanja) Matic na Jeremie Boga (kiungo wa kikosi cha chini ya miaka 21) ndio watakao kuwa nguzo ya kati kwa miaka 10 ijayo.
“Mradi ulioko ni kutayarishia mwongo ujao si musimu ujao. Unaweza dai kuna John Terry na Didier Drogba. Hao ni tofauti kwani Drogba ni straika aliyekuja kusaidia na kushabikia timu na hakuna beki bora Uingereza kama Terry licha ya umri wake,” Mourinho ambaye alisema Lampard angekuwa kizuizi cha kuimarisha kikosi chake alitangaza.

“Mchezaji mkubwa kama Frank angelikaba maendeleo ya vijana wengine. Ni maisha yake, aliondoka kama wakala huru na hatuwezi lalamikia hilo.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA