NEYMAR AANZA UFALME HISPANIA, MESSI AREJEA KWA 'GUNDU' AKOSA PENALTI

Winner: Neymar's goal in the first leg sealed his first trophy in Barcelona colours after his summer move
NYOTA wa Brazil, Neymar (Pichani) ameshinda taji lake la kwanza Barcelona kufuatia vigogo hao wa Katalunya kutwaa taji la nne la Super Cup ya Hispania ndani ya miaka mitano kwa faida ya bao la ugenini, baada ya sare bila kufungana 0-0 usiku wa jana Uwanja wa Nou Camp.


Baada ya sare ya 1-1 wiki iliyopita Uwanja wa Calderon, bao la Barca likifungwa na Neymar, aliyetokea benchi kuisawazishia timu hiyo mjini Madrid, alianzishwa katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo majira haya ya joto akitokea Santos ya kwao.

Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi pia alirejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi, lakini wote walishindwa kutikisa nyavu za wageni.

Messi alikosa hadi penalti baada ya kugongesha mwamba na mpira ukarejea uwanjani.

Katika mchezo huo, wachezaji wawili walitolewa nje kwa kadi nyekundu, Filipe Kasmirski dakika ya 80 na Arda Turan dakika ya 90 na ushei.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Victor Valdes, Dani Alves, Gerard Pique, Javier Mascherano, Jordi Alba, Sergio Busquets, Xavi, Cesc Fabregas/Andres Iniesta dk73, Alexis Sanchez/Pedro dk65, Neymar na Lionel Messi.Atletico Madrid: Thibaut Courtois, Miranda, Diego Godin, Luis Filipe, Juanfran, Gabi, Koke/Leo Baptistao dk89, Mario Suarez, Arda Turan/Adrian dk72, Diego Costa, David Villa/Cristian Rodriguez dk84.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA