MWAISABULA APINGA PENALTI YA COASTAL

Mkwaju wa penalti wa dakika za mwisho waliopewa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga na Mwamuzi Martin Saanya, umepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa soka nchini.


Kocha mzoefu, Kenned Mwaisabula "Mzazi" (Pichani) aliuambia mtandao huu jana kuwa mwamuzi hakustahili kutoa pigo la penalti kwa Coastal kutokana na umbali aliokuwepo wakati tukio likitokea.

“Saanya (Martin) hakustahili kutoa penalti ile kwa Coastal. Nasema hivi kutokana na umbali aliokuwepo wakati tukio lile linafanyika. Nadhani alikuwa umbali wa mita 15.”

“Kwa maana hiyo mwamuzi wa pembeni ndiye aliyekuwa karibu na tukio lile, lakini hakuonyesha alama yoyote kuashirikia kuna tukio limefanyika.”

Hata hivyo, kocha wa Yanga, Ernie Brandts alikiri kuwa penalti hiyo ilikuwa halali na hana sababu ya kuipinga, lakini ameshutumu kadi nyekundu ya  Simon Msuva.

Wakati huohuo, Klabu za Yanga na Coastal Union zimejiweka kwenye hatari ya kulimwa faini ya Sh500,000 kila moja baada ya wachezaji wake kupata kadi zaidi ya tano katika mchezo baina ya timu hizo.

Kwa mujibu wa kanuni ya 27 ya udhibiti wa wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania kifungu (d), timu ambayo wachezaji wake wataonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja itatozwa faini ya Sh500,000.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA