AZAM TV KUANZA SEPTEMBA

clip_image001 
Mashabiki wa soka wa Tanzania Bara wataanza kuishuhudia Ligi Kuumoja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha Azam TV katikamzunguko wa nne sambamba na tiketi za elektroniki.

Awali mechi hizo zlilipaswa kuanza kuonyeshwa leo wakati ligi ikianza, lakini kutokana na
kutosainiwa kwa mkataba rasmi, sasa zoezi hilo limesimamishwa mpaka katika mzunguko wa nne kupisha umaliziaji wa mazungumzo baina ya TFF na uongozi wa Azam.
Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa nakubaliano kati ya pande hizo mbili yalifikiwana na ukasainiwa mkataba wa awali ambao si rasmi (MoU) na kutakiwa
kusainiwa mwingine ambao utaruhusu urushwaji wa mechi ‘live’.
Katika hatua nyingine Wambura alisema tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda
ya tiketi imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi za kielektroniki hizo katika viwanja vyote.
“Hivi sasa Serikali ambayo ndiyo inamiliki Uwanja wa Taifa, TFF pamoja na CRDB
zinashughulikia mfumo wa tiketi hizo kwenye uwanja huo ambao ndiyo ulikuwa haujakamilika kwa matumizi katika upande huo,” alisema Wambura.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA