MAN UNITED, CHELSEA HAKUNA MBABE
Klabu za Chelsea
na Manchester United zimeminyana uwanjani Old Trafford. Pande zote
mbili zimekosa kufunga bao, na hivyo kutoka sare ya bila kwa bila.
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, wote wamepoteza pointi katika siku kumi na sita za kwanza wa msimu huu, na zinaifuata Manchester City iliyopoteza pointi pia kufuatia mechi dhidi ya Cardiff.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliiambia BBC Sport " Hakuna Upande uliostahili kushinda na kushindwa vile vile, unataka kushinda lakini pande zote zilikua na ulinzi mkali. Na kwa mashabiki najua angalau bao moja lingewafurahisha, iwapo ungekuwa mchuano mzuri''.
Naye meneja wa Manchester United, David Moyes alisema, alivunjika moyo kwa sababu hawakuzoa pointi yoyote, lakini ndivyo ilivyo na hawana budi kujifunza kutokana na hali hiyo.
Chelsea kwa sasa inaongoza ligi kuu kwa pointi saba, ikifuatwa kwa karibu sana na Liverpool na Tottenham, zote zikiwa na pointi sita. Machester United inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi nne.