KUMEKUCHA ULAYA: ARSENAL, MAN CITY WATAWEZA?

Timu ya Arsenal (Pichani) huenda ikawa na kibarua kigumu katika mechi za kutafuta nafasi ya kujitosa katika duru ya muondoano ya kombe la klabu bingwa bara ulaya.

Katika mechi za makundi vijana wa Arsene Wenger wamepangwa kundi moja na Borussia Dortmund ya Ujerumani, Olympic Marseille ya Ufaransa na Napoli kutoka Italy.
Arsenal waliingia katika duru ya makundi baada ya kuibandua timu ya Fenerbahce 5-0 katika mechi za mchujo zilizochezwa ugenini na nyumbani.
Timu nyegine ya Uingereza itakayo kuwa na wakati mgumu katika mechi hizo za makundi ni Celtic ya Scotland kwani imepangwa kucheza na mibabe ya soka Barcelona, AC Milan ya Italy na Ajax ya Uholanzi.
Jee Man City wataweza safari hii
Manchester City nao watalazimika kupepetana na bingwa wa kombe hilo la klabu bingwa ,Ulaya Bayern Munich, CSKA Moscow na Viktoria Plzen. Wapenzi wengi wa soka wanajiuliza je safari hii baada ya kupata kocha mpya mwenye uzoefu katika michuano hiyo ya kombe la klabu bingwa Manuel Pellegrini,Man City wataweza kupiga hatua na kuingia katika mechi za muondoano?
Kwa upande mwengine Kocha mpya wa Manchester United ,David Moyes hatakuwa na kazi kubwa sana kwani watapepetana na Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen ya Ujerumani na Real Sociedad ya Uhispania.
Miongoni mwa timu za Uingereza ni Chelsea peke yake ndio yenye kazi nyepesi kwani katika kundi lao watamenyana na Schalke ya Ujerumani, FC Basel na Steaua Bucharest.
Mechi za kwanza za makundi zinapaswa kugaragawa kati ya Septemba17-18 mwaka huu.

Orodha kamili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Group A: Manchester United, Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen, Real Sociedad
Group B: Real Madrid, Juventus, Galatasaray, FC Copenhagen
Group C: Benfica, Paris St-Germain, Olympiakos, Anderlecht
Group D: Bayern Munich, CSKA Moscow, Manchester City, Viktoria Plzen
Group E: Chelsea, Schalke, FC Basel, Steaua Bucharest
Group F: Arsenal, Marseille, Borussia Dortmund, Napoli
Group G: Porto, Atletico Madrid, Zenit St Petersburg, Austria Vienna
Group H: Barcelona, AC Milan, Ajax, Celtic

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA