DHAIRA AIBEBA SIMBA, MWAMUZI AINYONGA YANGA, JKT RUVU KUKAMATA USUKANI
Kipa Mganda Abel Dhaira ambaye alishutumiwa kwa makosa yaliyoifanya Simba ishikiliwe kwa sare katika mechi ya ufunguzi, jana alidaka penalti na kuisaidia Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Oljoro mkoani Arusha, wakati jijini Dar es Salaam penalti ya Jerry Santo iliinyima Yanga pointi tatu katika sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Azam, ambayo katika mechi ya ufunguzi ilitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, jana ilijiimarisha kwa ushindi wa magoli 2-0 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, kupitia magoli Gaudence Mwaikimba (dk. 56) na Seif Karihe (dk.78).
Kwenye Uwanja wa Taifa, mabingwa Yanga ambao walianza msimu kwa kishindo kwa kuisambaratisha timu ngeni kwenye ligi ya Ashanti kwa magoli 5-1, walidhani kwamba wamepata ushindi wa pili mfululizo wakati mshambuliaji wao Mrundi Didier Kavumbagu alipowafungia goli pekee katika dakika ya 70 kufuatia juhudi binafsi za beki David Luhende aliyempikia mfungaji.
Hata hivyo, katika dakika ya 90, mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro aliamuru penalti baada ya Luhende kuunawa mpira katika eneo la hatari na kiungo wa zamani wa Simba, Mkenya Jerry Santo kuwasawazishia Wagosi wa Kaya na kuzua hasira kwa mashabiki wa Yanga.
Mapema katika dakika ya 74, Saanya pia aliwatoa kwa kadi nyekundu wachezaji Simon Msuva wa Yanga na Chrispine Odula baada ya kugombana uwanjani.
Baada ya mechi kuisha mashabiki wa Yanga walianza kurusha mabarafu uwanjani kuelekea kwa mwamuzi Saanya, ambaye alitoka uwanjani chini ya ulinzi wa polisi, huku nje ya uwanja polisi wakilazimika kutumia mabomu kuwatawanya mashabiki ambao walikuwa wakipinga penalti hiyo ya dakika ya mwisho.
Mkoani Arusha, Oljoro JKT ndiyo walikuwa wa kwanza kuwasili uwanjani saa 9:11 wakiwa kwenye basi dogo aina ya Toyota Costa na dakika 18 baadaye, wageni wao, Simba waliingia kwenye uwanja huo uliojengwa 1977 wakiwa kwenye basi lao kubwa walilopewa na wadhamini wao, Kilimanjaro.
Katika hali ya kushangaza, baada ya basi la Simba kusimama ndani ya uwanja (karibu na mlango mkuu wa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo) ili wachezaji 'Wanamsimbazi' washuke, mzee mmoja, aliyekuwa ndani ya basi hilo alishuka na kumwaga maji yenye rangi nyekundu chini ya mlango wa basi hilo. Kila mchezaji alipokuwa akishuka, alikanyaga sehemu hiyo iliyomwagwa maji.
Mzee huyo aliyekuwa amevaa koti jeusi na suruali ya jeans bluu mpauko, pia aliiongoza timu hiyo hadi vyumbani akiwa ameshikilia chupa hiyo, ambayo bado ilikuwa na maji kidogo yenye rangi nyekundu.
Simba ilipata goli lake katika dakika ya 34 kupitia kwa Haruna Chanongo aliyefunga baada ya kukokota mpira kutoka katikati ya uwanja. Alipofika umbali wa takriban mita 22 kutoka langoni mwa Oljoro, alipiga shuti kali lililomshinda kipa Shaibu Issa ambaye ni dhahiri hakutegemea kama mfungaji angepiga shuti kutokea pale.
Babu Ally wa Oljoro alishindwa kuisawazishia timu yake katika dakika ya 57 baada ya penalti yake kudakwa na kipa Dhaira. Penalti hiyo iliamuriwa na refa Andrew Shamba kutoka Pwani baada ya Joseph Owino kumkwatua Issa Kandulu ndani ya boksi.
Dhaira ambaye mechi ya ufunguzi dhidi ya Rhino alifungwa magoli mawili ya kizembe, alikuwa mwiba kwa maafande jana akizuia kila hatari katika kiwango ambacho bila ya shaka ki
likuwa ni ujumbe kwa kocha Abdallah Kibadeni ambaye alisema baada ya mechi ya kwanza: "Tuna makipa watatu tutaangalia mechi ijayo tumchezeshe yupi.”
Baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho, mashabiki waliingia uwanjani kuwapongeza wachezaji. Askari wachache waliokuwapo uwanjani waliwahi kwa waamuzi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema anawapongeza vijana wake kwa kupambana ugenini na kupata pointi 3. "Mechi ilikuwa ngumu ukizingatia tumetumia wachezaji ambao bado hawajazoeana. (Mshambuliaji mpya Amisi) Tambwe hajafunga kwa sababu ni mgeni katika kikosi chetu na mfumo wetu pia," alisema Julio.
Kocha wa Oljoro, Fikiri Elias alisema kuwa marefa walichezesha vizuri lakini timu yake haikutumia vyema nafasi nyingi ilizozipata.Naye, George Chanda anaripoti kutoka mkoani Mbeya kuwa, wenyeji Mbeya City walipata ushindi wao wa kwanza tangu wapande daraja la Ligi Kuu baada ya kuifunga Ruvu Shooting kwa magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Paul Nonga aliifungia Mbeya City goli la kuongoza katika dk. 7 baada ya kuwatoka walinzi wa Shooting na kupiga shuti kali lililoenda moja kwa moja wavuni, kabla ya Shaban Suzan kuwasawazishia Shooting katika dk. 24 akiunganisha krosi kutoka kwa beki wa kushoto Stephano Mwasika.
Wakati watazamaji wakidhani mechi hiyo ingemalizika kwa sare ya bao 1-1, Steven Mazanda bao la pili dk 90 kwa shuti kali kufuatia pasi murua ya Alex Seth.
Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, alisema watazamaji wapunguze jazba kwa wachezaji wao kwa vile ligi bado changa.
Katika mechi nyingine, wageni wa ligi Ashanti walikumbana na kipigo cha pili mfululizo baada ya kuchapwa goli 1-0 dhidi ya JKT Mgambo ugenini Mkwakwani, Tanga lililofungwa na Fully Maganga katika dakika ya 62. Katika mechi yao ya kwanza, Ashanti walikaribishwa kwa magoli kipigo cha magoli 5-1 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa.
Mtibwa Sugar waliwafunga ndugu zao Kagera Sugar kwa goli 1-0 lililofungwa na Masoud Ali katika dakika ya 73 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Kipigo kikali cha jana kilikuwa ni kutoka JKT Ruvu waliowasambaratisha Prisons ya Mbeya kwa magoli 3-0 yaliyofungwa na Machaku Salum (dk.44), Emmanuel Swita (dk.69) na Hussein Bunu (dk.87).
Kwa ushindi huo, JKT Ruvu ambayo katika mechi ya awali iliifunga Mgambo 2-0, ilikwea kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi sita ikifuatiwa na timu za Yanga, Coastal, Azam, Simba, Mtibwa na Mbeya City zenye pointi 4 kila moja zikiachana kwa tofauti nzuri ya magoli.Vikosi:
Oljoro: Shaibu Issa, Yusuph Machogote, Napho Zuberi, Nurdin Mohamed, Shaibu Mayopa, Babu Ally, Swalley Iddy, Hamis Swallehe, Amiri Omari, Sabri Alli, Essau Sanu
Simba: Abel Dhaira, Nassoro Masoud 'Chollo', Issa Rashid,Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Amisi Tambwe, Haruna Chanongo.
Yanga: Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Salum Telela, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
Coastal: Shabani Kado, Juma Hamad, Abdi Banda, Marcus Ndehela, Juma Nyoso, Jerry Santo, Uhuru Seleiman, Chrispine Odula, Yayo Lutimba, Haruna Moshi 'Boban' na Daniel Lyanga.