BIG MECHI ULAYA, YAFUTA PAMBANO LA SIMBA MAFUNZO JUMAPILI
Mechi ya Simba na Mafunzo imesogezwa mbele mpaka Jumatatu ijayo ili kuwapa fursa mashabiki wa soka nchini kushuhudia mechi ya upinzani ya Ligi Kuu ya England kati ya mahasimu Liverpool na Manchester United itakayochezwa kesho alasiri.
Kocha Mkuu wa Mafunzo, Mohamed Shaaban, amesema wameamua kuja kucheza na Simba ili kuwapa uzoefu wachezaji ili waweze kucheza kwa mafanikio michuano ya Ligi Kuu Zanzibar.
Muandaaji wa mechi hiyo, George Wakuganda alisema kuwa, wameamua kusogeza mchezo huo hadi Jumatatu kwa lengo la kutoa fursa kwa mashabiki wa soka kuangalia mechi hiyo ya England Jumapili.
Wakuganda alisema, mchezo huo wa Jumatatu utachezwa saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumzia mchezo huo, Shaaban alisema: “Unajua mechi ya Simba ni muhimu kwangu kwa sababu itanipa heshima Zanzibar.”
“Wachezaji wengi wa Mafunzo ni vijana hawana uzoefu, ndiyo maana nikatafuta mechi ngumu kama hii ya Simba na malengo yangu ni kuwatoa woga. Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wenye majina kama hao Warundi (Kaze na Tambwe) na wengine, sasa kama watawamudu, tukirudi Zanzibar kucheza mechi za ligi watakuwa wameiva,” alifafanua Shaaban. Wachezaji chipukizi anaowazungumzia ni Amour Ally, Eddy Salum.