AKINA BALOTELLI WAFUZU HATUA YA MAKUNDI ULAYA

Wachezaji wa AC Milan
AC Milan ya Italia kwa mara ya kumi na moja katika muda wa miaka kumi na mbili iliyopita imefuzu kushiriki Kombe la Klabu Bingwa baranai Ulaya.

Milan imeilaza PSV Eindhoven kutoka Uholanzi kwa mabao 3-0.
Baada ya kutoka sare ya 1-1 na Uholanzi katika mechi ya awamu ya kwanza, Kevin Prince alifunga mabao mawili yaliyoiweka timu yake mbele, naye Mario Balotelli akaongezea la tatu na hivyo kuihakikishia mabingwa wa zamani wa kombe hilo nafasi katika raundi ijayo kwa jumla ya mgoli 4-1.
Katika matokeo mengine iliyochezwa siku ya jumatano, Zenit St Petersburg iliikwaruza Pacos Ferreira kwa mabao manne kwa mawili na kufuzu kwa hatua ijayo kwa jumla magoli manane kwa matatu.
Kwingineko, mabingwa wa Jamhuri ya Czech, Viktoria Plzen walishinda wenyeji wao Slovenia Maribor kwa bao moja kwa bila na kujikatia tikiti ya raundi ijayo ya makundi ya kinyang'anyiro cha kuwania Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya.
Viktoria Plzen imesonga mbele na jumla la magoli 4-1.
Klabu hizo zitajiunga na Arsenal Schalke, Steaua Bucharest na Austria Vienna ambazo zote zilishinda mechi zao siku ya Jumanne katika hatua ya makundi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA