XAVI AMKANA BALE, ADAI THAMANI HAIWEZI KUFIKA MILIONI 90
Kiungo huyo wa Hispania amenukuliwa akisema kwamba bado hajamuangalia vizuri nyota huyo wa Spurs kiasi cha kumfanya kutoa maoni yake kuhusu kutakiwa kwake na Real Madrid.
Alisema: “Sidhani kama Bale ana thamani ya fedha hizo zinazotajwa.
“Kiukweli kabisa sijawahi kumuona akicheza dakika 90 zote.”
Xavi pia alisisitiza Cesc Fabregas ana furaha kuwepo ndani ya Barcelona, pamoja na kutakiwa na Manchester United.
Kiungo huyo alisema: “Anaonekana kutulia, ana mkataba hapa. Anajituma mazoezini na anacheza vizuri.
"Kuhusu kuondoka, nadhani ni tetesi tu. Tutaona kitakachotokea lakini kwa sasa anaonekana kutulia na tayari kwa msimu mpya na Barcelona.”