WACHEZAJI WA NIGERIA WAPIGWA MARUFUKU MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA

Wachezaji na maafisa wa vilabu waliohusishwa na kupanga mechi ambazo hatimaye zilimalizika kwa mabao 79-0 na 67-0 wamepigwa marufuku maisha

Kilabu cha Plateau United Feeders walishinda mchuano wako kwa mabao 79-0 dhidi ya kilabu cha Akurba FC wakati kilabu cha Police Machine FC kilipoibwaga Bubayaro FC kwa mabao 67-0.
Vilabu hivyo vimepigwa marufuku kushiriki michauno yoyote kwa miaka 10.
Kamati moja ya Shirikisho la soka la Nigeria ilipendekeza kuwa maafisa wa soka waliohusika katika upangaji huo wa michuano miwili kupigwa marufuku maisha.
Plateau United Feeders na Police Machine waliingia kwenye mechi yao wakiwa na pointi sawa huku wakiwa katika hatari ya kuvuka na kuingia daraja ya chini ya ligi ya kitaifa ikiwa wangepoteza mechi .
Feeders ilishinda kwa mabao 72 katika kipindi cha pili cha mechi, wakati Police Machinen nao wakipata mabao 61 baada ya kipindi cha mapumziko.
Matokeo hayo yalimaanisha kuwa Plateau ilipanda daraja juu ya Police Machine kwa toafuti ya mabao.
Shirikisho la soka Nigeria limesema kuwa limekubali mapendekezo hayo na kuwa litawasiliana na vilabu husika, pamoja na FIFA.
Shirikisho hilo lilisema litachapisha majina ya wachezaji , picha zao na maelezo kuwahusu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA