SIMBA YAWAFUATA BOBAN NA NYOSSO TANGA

SIMBA SC inasafiri hadi Tanga kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kujiandaa na msimu, itakapomenyana na wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani kesho jioni.

Hiyo itakuwa ziara ya nne kwa Simba SC katika kipindi hiki cha majira ya joto, baada ya awali kwenda Katavi, Shinyanga na Mara.
Wekundu hao wa Msimbazi, chini ya kocha wao mpya, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ wamekwishacheza mechi tano na kati ya hizo wameshinda tatu, sare moja na kufungwa moja.

Waliifunga Rhino Rangers iliyopanda Ligi Kuu mabao 3-1 na baadaye Kombaini ya Katavi 2-1, Kahama United 1-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Polisi Mara na kisha kufungwa 2-1 na URA ya Uganda mjini Dar es Salaam.
Kwa Coastal, tangu waanze maandalizi ya msimu wamecheza mechi moja na URA Jumatano na kuibuka na ushindi wa 1-0, Uwanja wa Mkwakwani.
Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa mzuri- kwani utakuwa wa kwanza kwa Coastal kucheza na Simba tangu iwasajili wachezaji waliotupiwa virago Msimbazi, Juma Nyosso na Haruna Moshi ‘Boban’ (Pichani juu). 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA