ROONEY SASA KUTUA ARSENAL
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney (Pichani) ataamua kwenda Arsenal iwapo tu ndoto zake za kufanya kazi na Jose Mourinho Chelsea litabuma.
Manchester United imekataa kumuuza
Rooney kwa wapinzani wake wakuu kwenye mbio za ubingwa, lakini
mshambuliaji huyo bado anataka kuondoka Old Trafford.
Pamoja na kwamba Chelsea ni chaguo la
kwanza, mshambuliaji huyo wa England atakwenda Arsenal iwapo David Moyes
na bodi ya United itakaata ofa nyingine ya Mourinho.
Anaondoka? Wayne Rooney anatakiwa na Arsenal na Chelsea
Arsenal ilitia mkono kwa Rooney, ambaye
atatimiza miaka 28 mwaka huu, wakati alipowekwa benchi katika mazingira
ya kutatanisha kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa nyumbani
dhidi ya Real Madrid, Machi.
Arsenal imesema inaweza kulipa mshahara
wa Rooney, anayelipwa Pauni 240,000 kwa wiki na amebakiza miaka miwili
katika Mkataba wake wa sasa.
Chelsea wanabaki kileleni katika
ushindani wa ofa kubwa, wakiwa wametoa Pauni Milioni 23, jumlisha Pauni
2.5 zitakazoongezwa kwa vipengele.
Baada ya kuumia nyama, Rooney alirejea
kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa United, Carrington na ni
matumaini klabu hizo mbili zitafikia makubaliano. Mkewe, Coleen
anafurahia maisha ya London na mtoto wao kwa manufaa ya kazi yake.
Ushindani: Jose Mourinho na Arsene Wenger wote wanapenda kumsaini Rooney kutoka United
Ubora wa nyota huyo ndio unaomfanya Mourinho ajaribu kumhamishia Rooney Chelsea, lakini pia anamheshimu Arsene Wenger.
Mshambuliaji huyo wa England, ambaye
anaweza kuwa fiti kucheza wiki mbili zijazo, ameambiwa kocha wa Arsenal,
Wenger atajenga timu yake kwa kumhusisha yeye.
Hiyo inafuatia Rooney kusukumwa nje ya
kikosi cha kwanza na Sir Alex Ferguson na hadhi yake kushuka chini ya
kocha mpya, David Moyes.
David Moyes yuko kwenye hatari ya kupoteza moja ya nyota wake
Rooney alifanya mawasiliano ya simu
Moyes na Makamu Mwenyekiti, Ed Woodward baada ya kuibuka taarifa kwamba
mshambuliaji huyo amekasirika kutokana na namna anavyochukuliwa katika
klabu hiyo.
Chelsea inajiandaa kuongeza ofa yake kwa
ajili ya Rooney, lakini haitakuwa tayari kuzidisha Pauni Milioni 30.
Ikiwa United itakataa kumuuza Chelsea- Arsenal watakuwa kwenye nafasi
nzuri ya kumpata.