OWINO AIBUKIA ULINZI YA KENYA
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya mwaka 2010 (KPL) Ulinzi Stars
wameteua kikosi kikali cha wachezaji 20 kinachochanganya ujana na ujuzi
kwa ajili ya Michezo ya Wanajeshi Afrika Mashariki itakayoandaliwa
Nairobi wiki ijayo.
Nahodha Evans Amuoka ataongoza kikosi hicho ambacho pia kinajumuisha mchezaji aliyejiunga nao majuzi Fred Chitai na kipa asiyejulikana sana Fineas Odhiambo.
Hayo yanajiri chini ya wiki tatu baada ya wanajeshi hao kushiriki Michezo ya Wanajeshi ya Dunia mjini Baku, Azerbaijan ambapo walishindwa kufuzu kutoka ngazi ya makundi. Lakini ushindi wao mara mbili hivi majuzi kwenye ligi ya nyumbani dhidi ya Chemelil Sugar na Nairobi City Stars unawapa motisha wanapoelekea kwenye dimba hilo.
Kwa mujibu wa mkuu wa timu hiyo Meja Erick Oloo, timu hiyo iko tayari kupigania taji ambalo walipoza pembamba kwa Uganda mwaka uliopita nchini Rwanda.
“Tuko tayari wakati huu kushinda taji. Kuwa wenyeji wakati huu pia kutatufaa zaidi na tunalenga kushinda. Mwaka uliopita, Uganda walitushinda kwa wingi wa mabao lakini tunawaambia watarajie kibarua wakati huu,” Meja Oloo aliambia tovuti rasmi ya klabu hiyo.
Baada ya mechi ya ligi Jumamosi dhidi ya AFC Leopards, klabu hiyo yenye makao yake Nakuru itapewa ruhusa kwenda kushiriki dimba hilo la eneo la Afrika Mashariki.
“Baada ya mechi dhidi ya AFC Leopards mnamo Jumamosi, tutaingia kambini kujiandaa kwa michezo hiyo na mechi itakayofuata ya KPL ambayo itakuwa Agosti 14 dhidi ya Karuturi mjini Naivasha,” akaongeza Meja Oloo.
Kikosi: Francis Ochieng, Franklyn Miheso, Fineas Odhiambo, Fred Chitai, Mohammed Hassan, Mulinge Ndetto, Geoffrey Kokoyo, Josiah Okello, Oliver Kiprutto, Amon Mwamburi, Mohammed Abulala,Stephen Ochollah,Antony Muriithi, Collins Ochieng, Lawrence Owino, Kelvin Amwayi, Salim Mohammed, Oliver Agwanda, Evans Amwoka na Stephen Waruru.