MKIMBIAJI KENYA AZIRAI UWANJANI

Cheptai akipewa huduma ya kwanza
Mwanariadha wa Kenya wa mbio za masafa marefu Irine Chebet Cheptai amekimbizwa hospitalini baada ya kuzirai katika mbio za uwanja wa Olimpiki.
Cheptai ambaye alikuwa kuwa mmoja wa wanariadha walioshiriki katika mbio za mita elfu tatu alizirai muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo ambapo alimaliza katika nafasi ya kumi na moja na kuweka muda wake kasi zaidi katika mbio hizo wa dakika nane na sekunde ishirini. Madaktari waliokuwa uwanjani walimtibu mwanariadha huyo aliyekuwa amepoteza fahamu kabla ya kumkimbiza hospitalini kwa machela.
Ripoti zinasema Cheptai hatimaye alipata fahamu akipokea matibabu hospitalini.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka ishirini na moja hushiriki katika mbio za mita elfu tano na mwaka huu tayari ameshiriki katika mashindano mawili ya dunia ya IAAF Diamond League.
Mwezi Mei mwaka huu mjini Shanghai, Cheptai aliandikisha muda wa dakika kumi na nne sekunde hamsini nukta tisa tisa, muda ambao ndio bora zaidi aliouandikisha katika mbio hizo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA