KING MAJUTO AIBUKA TENA NA MBOTO
Katika filamu hiyo iliyoandaliwa na Salma Jabu 'Nisha' na kuandikwa na kuongozwa na Leah Richard 'Lamata', King Majuto kama kawaida yake anavunja mbavu mwanzo mwisho akishirikiana na Haji Salum 'Mboto' na wakali wengine walioigiza pamoja.
Kwa mujibu wa Lamata, mbali na Majuto na Mboto, filamu hiyo imewashirikisha pia Hemed Suleiman 'PHD', Chuchu Hans, Jacklyne Wolper na wengine.
"Ni bonge la filamu ambalo karibu waigizaji wote wametikisa kama lilivyo jina la filamu yenyewe, ni moja ya kazi nzuri nilizowahi kuziandika na kuziongoza baada ya kutoka na 'Poor Minds' na 'Pain Killer'," alisema Lamata.