KABURU SASA KUMVAA RAGE

ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (Pichani) , amesema ana imani bado ana umuhimu katika klabu hiyo na atashiriki uchaguzi ujao kama Mungu atamjalia uzima na afya.


Kaburu alijing’atua miezi kadhaa iliyopita kwa kutoridhishwa na baadhi ya mambo ya kiutendaji katika klabu hiyo huku nafasi yake ikizibwa na Joseph Itang’are ‘Kines’ anayekaimu.

Alisema kwa vile alijiondoa mwenyewe, hivyo anao uwezo wa kurudi endapo atataka kurudi kipindi cha uchaguzi ujao.

“Mimi hakuna aliyeniondoa Simba, ila kutokana na kutoridhishwa na utendaji kutoka kwa wenzangu na mimi nikiwa kama kiongozi wa juu nikaamua nijiweke kando niwaache,” alisema Kaburu kiongozi aliyeisaidia Simba katika mambo mbalimbali ikiwemo usajili.

Aliongeza kuwa hatosita kuisapoti klabu hiyo, kwa namna yoyote ile kwa kuwa bado ni mwanachama halali wa klabu hiyo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA