HASSANOO SASA JELA INAMUITA
Makogo alitoa ushahidi wake jana mbele ya Hakimu Devotha Kisoka. Mawakili wa upande wa Jamhuri waliongozwa na wakili mwandamizi wa serikali, Tumaini Kweka huku upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili Richard Rweyongeza na Majura Magafu.
Shahidi huyo alidai kuwa siku ya tukio alipigiwa simu na Rahimu Jeta ambaye ni mkurugenzi wake na kuambiwa kwamba kuna gari lililotoka Zambia kuja Dar es Salaam linaonekana limepaki pembeni ya barabara na lilikuwa wazi bila mizigo.
Shahidi huyo alidai kwamba alikuwa ameongozana na dereva wa gari lake, Abdalah Kota na wakaenda kituo cha polisi kuomba kuongozana hadi katika mahala lilipokuwa gari hilo aina ya Scania lenye namba T821 DCL.
Alidai kwamba alipigiwa simu na Jeta aende kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay na baada ya hapo wakaongozana na polisi hadi Bahari Beach, kwenye Yard ya Najim na kukuta madini ya shaba yaliyokuwa yakitoka Zambia kuja Tanzania huku yakiwa yamefunikwa turubai jekundu.
Aliieleza mahakama kuwa waliangalia kwenye mfumo wa ufuatiliaji kwa njia ya kompyuta, na kuona gari lilifika jijini usiku na kuelekea hadi eneo hilo ambalo shaba hiyo ilipelekwa badala ya bandari kavu.