BAYERN MUNICH YAIPA CHELSEA PAUNI MILIONI 40 KWA AJILI YA DAVID LUIZ
KLABU ya Bayern Munich imepanga kufufua mpango wa kumsajili David Luiz (Pichani) na imeandaa dau la Pauni Milioni 40 kuhakikisha inamnasa.
Kocha wa Bayern, Pep Guardiola anaona
beki huyo wa kati atasaidia sana kuimarisha ukuta wa mabingwa hao wa
Ulaya na kwa muda mrefu amekuwa akimzimikia Luiz.
Chelsea ilimtuliza beki huyo Mbrazil
mwenye umri wa miaka 26, kwa kumsainisha Mkataba mpya wa miaka mitano
Septemba mwaka jana, na imesema hauzwi na kocha Jose Mourinho alijaribu
kupuuza maoni kwamba Luiz si aina ya beki wa kati wakati wa ziara ya
timu hiyo Asia.
Hakuna mpango: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekanusha madai kwamba Luis hafai kuwa beki wa kati kwake
Maelekezo: Kocha wa Bayern, Pep Guardiola anataka kuimarisdha safu yake ya ulinzi