BARCELONA YASISITIZA FABREGAS HAUZWI

Cesc Fabregas

Naibu rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesisitiza kuwa Barcelona haitamuuza Cesc Fabregas kwa Manchester United, bila kujali bei.

Akiongea wakati wa kutambulishwa kwa kocha mpya Gerardo Martino mnamo Ijumaa, Bartomeu alisema “haijalishi ni pesa ngapi Manchester United wako tayari kutoa, lakini hatutamwachilia aende. Tunamtegemea.”
Wiki iliyopita United waliahidi kulipa Euro 30 milioni ($39 milioni) kumrejesha nahodha huyo wa zamani wa Arsenal mwenye umri wa miaka 26 katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Bartomeu anasema klabu hiyo ya Uhispania “haitatizwi” na juhudi za United kutaka kuponyoka na kiungo huyo wa kati. Anasema ni “kawaida kwamba wanamezea mate Cesc. Ni mchezaji nyota.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA