BARCELONA YAMTANGAZA GERARDO MARTINO KUWA KOCHA MPYA, SASA KUENDELEZA PASI ZA VILANOVA
KLABU ya Barcelona imefikia makubaliano na Muargentina, Gerardo Martino (Pichani) kuwa kocha wao mpya.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50,
ambaye aliiongoza Old Boys ya Newell kutwaa taji la Clausura Argnetina
msimu uliopita, amekubali Mkataba wa miaka wa miaka miwili Barca ambako
anakwenda kurithi mikoba ya Tito Vilanova.
Barca ilitangaza Ijumaa usiku kwamba, Vilanova mwenye umri wa miaka 44 amejiuzulu ili kuendelea kupata matibabu ya saratani.
Mtu mpya: Barcelona imemchukua Gerardo Martino kuwa kocha wao mpya
Ameachia ngazi: Tito Vilanova amejiuzulu Barca ili kuendelea kupata tiba ya saratani
"FC Barcelona imefikia makubaliano na
kumteua Gerardo Martino kuwa kocha mpya wa timu ya soka kwa misimu
miwili ijayo. Makubaliano hayo yanafutiwa na utayarishaji wa Mkataba na
kusaini,"imesema taarifa kwenye fcbarcelona.cat read.
"Saa zijazo [mipango ilivyo] akiwasili Barcelona, atasaini Mkataba na kutambulishwa mara,".
Makocha kadhaa wazawa walitabiriwa
kupewa kazi na mabingwa hao wa Hispania, wakiwemo Luis Enrique, Andre
Villas-Boas, Marcelo Bielsa, Michael Laudrup na Guus Hiddink, ambaye
jana amejiuzulu Anzhi Makhachkala.
Kocha wa nyumbani: Martino anatokea Rosario nchini Argentina, kama mfalme wa mabao wa Barcelona, Lionel Messi
Pamoja na hayo, Martino aliwapiku wote
hao na kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Argentina, amethibitishwa
leo kuwa kocha mpya.
Martino amekuwa kocha wa timu ya Newell
ya nyumbani kwao, Rosario kwa misimu miwili iliyopita na aliichezea
klabu hiyo kwa vipindi vitatu tofauti.
Pia amechezea Tenerife ya Hispania na Lanus ya nyumbani kwao, Barcelona SC ya Ecuador na O'Higgins ya Chile.
Kabla ya kuwa kocha wa Newell, Martino aliifundisha kwa miaka minne Paraguay, kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.
Aliiongoza timu hiyo kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 matokeo mazuri zaidi kwa nchi hiyo daima kwenye mashindano hayo - kabla ya kufungwa 1-0 kwa mbinde na Hispania, walioibuka mabingwa.
Aliiongoza timu hiyo kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 matokeo mazuri zaidi kwa nchi hiyo daima kwenye mashindano hayo - kabla ya kufungwa 1-0 kwa mbinde na Hispania, walioibuka mabingwa.
Martino aliifikisha Paraguay Robo Fainali Kombe la Dunia mwaka 2010
Wachezaji wa Barcelona, wakiwemo Carles
Puyol, Messi na kipa Jose Manuel Pinto walihudhuria mkutano wa kujiuzulu
kwa Vilanova ulioongozwa na Rais, Sandro Rosell (chini)
Mwaka ulipfuata, Martino aliiwezesha
Paraguay kutinga Fainali ya kwanza ya Copa America tangu mwaka 1979
ambako hata hivyo walifungwa 3-0 na Uruguay naye akajiuzulu mwezi mmoja
baadaye.
MJUE GERARDO MARTINO
1962: Alizaliwa Novemba 20 mjini Rosario, Argentina.
1980-90: Kiungo
huyo mshambuliaji anajiunga na Newell Old Boys ya Argentina na
kuichezea mechi 392 za ligi, akifunga mabao 35 ndani ya miaka 10.
Alitwaa taji la Primera Division mwaka 1988.
1991: Alicheza mwaka mmoja Tenerife na kuichezea mechi moja timu ya taifa yaArgentina chini ya Alfio Basile.
1991-94: Alirejea Newell Old Boys kwa miaka mitatu na kutwaa mataji mawili zaidi ya Argentina.
1994-95: Aliichezea kwa msimu mmoja Lanus kabla ya kurejea Newell Old Boys.
1996: Alikwenda Ecuadorian kuichezea mwaka mmoja Barcelona Sporting Club na kisha O'Higgins ya Chile.
1998: Alifanya kazi ya ukocha kwa mara ya kwanza Brown de Arrecifes.
1999: Alijiunga na Platense kama kocha.
2000: Alikuwa kocha Mkuu wa Instituto.
2002-03: Aliiongoza Libertad kutwaa mataji mawili ya Paraguay.
2004: Alitwaa taji la Paraguay akiwa na Cerro Porteno.
2005: Alikuwa kocha wa Colon kwa msimu.
2005-06: Alirejea Libertad na kutwaa taji la nne la Paraguay mwaka 2006.
2007: Februari - alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Paraguay na akashinda tuzo ya Kocha bora wa Mwaka Amerika Kusini.
2010: Juni - Aliiongoza Paraguay katika Kombe la Dunia Afrika Kusini na kuifikisha hadi Robo Fainali, ambako ilifungwa na Hispania.
2011: Baada ya Paraguay kufungwa katika Fainali ya Copa America na Uruguay, ajajiuzulu ukocha wa timu hiyo ya taifa.
2012-13: Alirejea Newell Old Boys kama kocha na kutwaa taji la Clausura mwaka 2013.
2013: Julai 23 - Anakubali Mkataba wa miaka miwili Barcelona, kurithi mikoba ya Tito Vilanova.