Wabunge wa Kenya wajiongeza mishahara

Wanaharakati nchini Kenya waliandamana kupinga njama ya wabunge kujiongeza mishahara

Wabunge nchini Kenya wamepiga kura kujiongeza mshahara na kwenda kinyume na tume ya kitaifa ya kuratibitisha mishahara ya maafisa wa serikali.

Kura hiyo waliyopiga bungeni hapo Jumanne itawawezesha sasa kupokea mishahara ya dola elfu kumi. Mshahara wa mkenya wa kipato cha kadri ni dola 1,700.
Rais Uhuru Kenyatta aliwaomba wabunge hao mapema mwezi huu kuruhusu mishahara yao kupunguzwa ili waweze kuiwezesha serikali kupata pesa za kutengeza ajira kwa wananchi.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wale wanaopokea mishahara mikubwa duniani na hatua yao ya kibinafsi imewaghadhabisha wakenya waliofanya maandamano kuwafananisha wabunge hao na Nguruwe kwa ulafi.
Lakini wabunge hao waliteta kuwa hatua ya kupunguza mishahara yao ni kinyume na sheria.
"wametupokonya utu wetu na lazima tuweze kuurejesha,'' alisema mbunge Jimmy Angwenyi bungeni.
Kura waliyopiga wabunge hao, itapingwa leo mahakamani na makundi ya kutetea haki za binadamu
Rais wa Kenya hana uwezo wa moja kwa moja kuratibu mishahara ya wabunge.
Tume ya kitaifa ya mishahara iliratibu mishahara ya wabunge hao na kusema kuwa watapokea dola 6,300.
Wabunge hao, awali walisema kuwa wanapaswa kulipwa dola elfu kumi baada ya kusema kuwa wanafanya kazi kwa bidii.
Wabunge katika bunge lililopita walijilimbikizia dola 107,000 kama marupurupu ya kustaafu katika moja ya vikao vyao vya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Machi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA