TUJIKUMBUSHE ZAMANI

MUSSA HASSAN MGOSI

Aliyefanikiwa kuzima ngebe za Yanga, Apigiwa chapuo arejeshwe Simba

Na Exipedito Mataruma

NI kweli klabu ya Simba haijawahi kuwa na straika mwenye bahati ya kuzima ngebe za Yanga kwa muda mrefu, Ni kweli Simba inahitaji mshambuliaji mwenye shabaha kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi.


Kipindi cha usajili kimefikia, Wachezaji ni wakati wao huu kunufaika kwani kila timu imekuwa katika harakati za kusuka upya kikosi chake ili msimu ujao wa ligi utakapoanza kusiwe na visingizio.

Lakini Tujikumbushe zamani kama zilivyo sera zetu Mwanasoka, Mwanzoni mwa mwaka 2000 na kuendelea klabu ya Simba ilikuwa ikiitawala sana Yanga hasa ndani ya uwanja na nje pia.

Simba ilikuwa ikiifunga Yanga kila wanapokutana na ilipelekea kuonekana jambo la kawaifda Simba kumfunga Yanga, Wapo baadhi ya wapenzi wa Yanga ambao walidiriki kukacha maudhurio ya mechi ya klabu yao inapocheza na Simba.

Na kama ulikuwa haujui sasa tambua hili, Mashabiki wa Yanga ndio watu wa kwanza kabisa hapa nchini kuanza kupenda timu za Ulaya, Mashabiki hao wa Yanga baada ya kuiona timu yao ikipoteza mwelekeo kwa vichapo mfululizo toka kwa Simba waliamua kushabikia ligi za Uingereza, Italia, Ujerumani na Hispania.

Si kwamba natania ila ndivyo ilivyo tafiti yangu na nyinginezo, Simba kulikuwa na raha sana tena kupita kiwango, Uongozi wake ulistawi vema wafadhili nao walijazana kiasi kwamba Simba iliwahi kufadhiliwa na kampuni nne kwa mkupuo.
Walianza benki ya NBC, Twiga Cement. Mohamed Interprises na Kilimanjaro Primiem Lager, Simba ilikuwa bonge la Simba, Lakini mashabiki wa Yanga walikuwa wakimuogopa zaidi mshambuliaji hatari wa Simba wakati huo Mussa Hassan M

Mgosi alikuwa na bahati ya kuitungua Yanga kila mara wanapokutana, Yanga ilibadili makipa lakini wote aliweza kuwatungua, Kuna kipindi Yanga ilimsajili kipa mzungu na siku walipokutana Mgosi alikosa goli la wazi lililopelekea shutuma dhidi yake.

Katika mchezo huo Yanga ilishinda 1-0 lililowekwa kimiani na Benny Mwalala ambaye kwangu mimi ninaamini ndiye mwokozi wao, Lakini katika mechi ya marudiano kichapo kiliendeleza kama kawa kwa Simba kumfunga Yanga.

Mgosi alifanikiwa kumtungua mzungu huyo na kuondoa uvumi uliozagaa kuwa Mgosi alikuwa akitumia ndumba na alishindwa kwa mzungu ambao awaamini imani za kishirikina.

MGOSI AKANA KUTUMIA NDUMBA

Mshambuliaji huyo wa kutegemewa wa Simba alikana kutumia ndumba na alisema kuwa kujituma ndio siri ya mafanikio kwake, Nyota yake ilizidi kung'ara ambapo alipata kuibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zaidi ya misimu miwili mfululizo.

Mgosi alipata kuitumikia timu ya taifa iliyokuwa ikinolewa na Mbrazil Marcio Maximo kocha mwenye falsafa ya kutopenda kukumbatia wachezaji wenye utovu wa nidhamu.

Lakini Mgosi alikuwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichofanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani yaani CHAN.

Fainali hizo zilifanyika nchini Ivory Coast ambapo katika fainali hizo Mgosi aliteuliwa katika kikosi bora cha wachezaji 11 wa CAF, Hiyo ni moja kati ya heshima ambayo anajivunia mchezaji huyo mkongwe.

Mgosi alianza kuchipukia katika ulimwengu wa soka akiwa na timu ya JKT Ruvu ya Mlandizi mkoani Pwani, Akicheza kwa malengo katika timu hiyo iliyokuwa moja ya timu machachari katika soka la Tanzania kutokana na ushindani wake iliokuwa ukiotoa kwa miamba ya soka nchini Simba na Yanga.

Mgosi alisajiliwa na Mtibwa Sugar ambapo hapo ndipo alipoanza kung'ara na baadaye kusajiliwa na Simba, Alicheza Simba kwamafanikio makubwa ambapo aliweza kushinda mataji mbalimbali yakiwemo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

EMMANUEL OKWI ALIJIFUNZA KUTOKA KWA MGOSI

Leo hii ukimtaja Emmanuel Okwi kuwa ni mmoja wa mastaa wa solka la Tanzania hasa klabu ya Simba lakini lazima umtaje Mgosi, Okwi alikuwa akisubiri kwa Mgosi.

Na alikuwa akijifunza mengi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa kutegemewa wa zamani katika klabu ya Simba, Simba ilipoona tayari Mgosi ameshaiva iliamua kumuuza kwa klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo ama DRC.

Akiwa DRC, Mgosi aliweza kuiongoza timu yao kufanya vizuri katika ligi kuu ya Kinshasa ingawa baadaye alikuja kushindwa kucheza sambamba kutokana na majeraha ya hapa na pale.

Msimu uliopita, Mgosi alirejea nyumbani ambapo ilikuwa ajiunge tena na Simba lakini ITC ilishindwa kukamilishwa haraka ambapo uongozi wa JKT Ruvu uliamua kumrejesha nyumbani alikotoka.

Mgosi alianza kuitumikia JKT Ruvu katika ligi kuu ya Vodacom iliyomalizka hivi karibuni na kuweza kuifungia magoli muhimu timu hiyo iliyosaidia kubakia katika ligi hiyo, JKT Ruvu ilikuwa katika nafasi mbaya ya kutelemka daraja.

Umuhimu wa Mgosi ulikuja kuonekana wakati alipoanza kucheza katika mzunguko wa pili, Mgosi alifanya kazi kubwa katika mechi yao iliyowakutanisha na Simba katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Simba ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 ambapo Mgosi aliweza kuwapa wakati mgumu Simba, Kwani juhudi zake binafsi zilizaa goli la kuongoza.

Anapigiwa debe na wadau na mashabiki wa Simba ili aweze kusajiliwa tena kwani kiwango chake bado kipo sawa sawa, Mgosi ajashuka kiwango kwani katika mechi zote alizocheza akiwa na JKT Ruvu alionyesha kumudu kabisa mikikimikiki ya ligi kuu.

Pia ataweza kushirikiana na chipukizi waliopo sasa Simba hivyo umuhimu wake bado unahitajika, Endapo Mgosi atarejea tena Simba anaweza kuzima tena ngebe za Yanga kama alivyofanya katika misimu iliyopita

gosi.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA