SUAREZ ASEMA KUIKATALIA REAL MADRID NI NGUMU
MSHAMBULIAJI
Luis Suarez amezua hofu juu ya mustakabli wake katika klabu ya
Liverpool baada ya kusema itamuwia vigumu kukataa ofa ya Real Madrid.
Suarez,
anayetumikia kifungo cha adhabu ya mechi 10 kwa kumng'ata beki wa
Chelsea, Branislav Ivanovic, amesema katika mahojiano na kituo cha Redio
cha Uruguay analazimika kuondoka kutokana na jinsi anavyoshambuliwa na
vyombo vya habari England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema: "Liverpool wanataka nibaki, lakini ngumu kuwakatalia Real Madrid.
"Nina familia ambayo pia inaathiriwa na hali hii na imevuka kiwango.
"Sijiandai
kupambana na Waandishi wa Habari wa England. Nimepambana sana tangu
nikiwa mdogo kufika hapa nilipo, kuwaacha waandishi fulani wanitendee
ubaya.
"Hawanihukumu
kama mimi ni mchezaji, bali mtazamo wangu. Wananizungumzia kana kwamba
wanafahamu maisha yangu yote vizuri. Nina mke na mtoto wa kike na siko
tayari kuendelea kupambana na vyombo vya habari vya England,"alisema.
Liverpool imesistiza Suarez hauzwi na kwamba kwa kuwa alisani mkataba mpya wa miaka minne msimu uliopita, wanatarajia atabaki.
Suarez kwa sasa yupo na timu yake ya taifa, Uruguay
Kocha
Brendan Rodgers hana presha ya kumuuza mchezaji huyo, lakini Madrid
wanaandaa Pauni Milioni 25 na wachezaji wawili, washambuliaji chipukizi
Alvaro Morata na Jese Rodriguez.
Liverpool
pia inakabiliwa na mtihani wa kumzuia kipa Pepe Reina anayetakiwa
Barcelona ambaye amesema wazi itakuwa vigumu kukataa ofa ya vigogo wa
Catalan.
"Ni
vigumu kuwakatalia Barca, pamoja na kwamba sina uhakika kama
wananihitaji kwa dhati,' alisema mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka
30.
Aspas amefanya vizuri katika msimu wake huu wa kwanza La Liga
Lakini
Liverpool imeimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kukubali kumsajili
kwa Pauni Milioni 6, mshambuliaji wa Celta Vigo, Iago Aspas, mwenye umri
wa miaka 25, ambaye anaweza kucheza katikati au pembeni.
Huku
Celta Vigo ikikabiliwa na hatari ya kushuka Daraja dau hilo ni punguzo
kutoka Pauni Milioni 8 na Aspas atafanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo.