SPURS YATOA PAUNI MILIONI 1O KUMSAJILI MKALI WA MABAO HISPANIA ALIYEFULIA BARCA
KLABU ya Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kwa Pauni Milioni 10, mshambuliaji wa Barcelona David Villa na pia wamefufua nia yao ya kumsajili mchezaji wanayemtaka kwa muda mrefu, Leandro Damiao.
Andre Villas-Boas aliibua nia ya
kumsajili ya Villa mapema mwezi huu na sasa klabu yake nchini Hispania
iko tayari kuisikiliza Spurs katika mpango wao wa kumnasa mkali huyo wa
mabao kwa ajili ya msimu ujao.
Klabu hiyo ya Nou Camp iko tayari
kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye amejikuta
katika wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza na anaweza
akauzwa kwa Pauni Milioni 12.
Atatua Spurs? Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa anatakiwa Tottenham kwa Pauni Milioni 10