REAL MADRID YATOA PAUNI MILIONI 40 KUMNASA SUAREZ
MSHAMBULIAJI Luis
Suarez inaonekana yuko njiani kuondoka Anfield baada ya jana usiku,
kuibuka madai kwamba Real Madrid imetoa ofa ya Pauni Milioni 40
kumhamishia Bernabeu.
Kiasi
cha saa 24 baada ya mpachika mabao huyo wa Liverpool kuiambia Redio ya
Uruguay itamuwia vigumu kuwakatalia Madrid wakimtaka, gazeti maarufu
Hispania, Marca limeripoti kwamba makubaliano yamefikiwa kumfanya awe
mchezaji wa Real.
Liverpool
wamekasirishwa na habari za kwamba Real imeanza mchakato wa kumsajili
Suarez bila kuwasiliana na klabu ya mchezaji huyo. Imesema Suarez
atakuwa amekiuka mkataba wake kufanya mazungumzo na Real bila ridhaa ya
klabu.
Suarez
pia amewaruka Marca juu ya taarifa yao, ingawa bado mustakabali wake
Anfield uko shakani. "Si kweli nina makubaliano na Real
Madrid. Nafikiria mustakabali wangu, lakini bado sijaamua
chochote,"alisema’
Rais
wa Real, Florentino Perez amemzungumzia mchezaji huyo na kusema:
"Suarez ni mchezaji mkubwa, na nina uhakika klabu zote duniani
zinamtaka. Nampenda,".