Poulsen aifua Stars mara 4 Ethiopia


TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) iliwasili hapa Ethiopia jana alfajiri kwa ajili ya kuanza kambi ya maandalizi ya kuwakabili Morocco (Lions of the Atlas) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.


Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na ilianza mazoezi jana saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Kwa mujibu wa kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi ya Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Sudan ambayo pia imeweka kambi yake mjini Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza juzi dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala kwa mabao mabao 2-0.

Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa 'Barthez', Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha, Amri Kiemba, Salum Abubakar 'Sure Boy', Simon Msuva, John Bocco, Vincent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd 'Chuji', Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu, ambapo itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA