KUTANA NA SHEDDY CLEVER

Picha ya kwanza Sheddy akiwa katika studio yake.
Picha ya pili Sheddy akiwa ameweka pozi katika studio yake ya Burn Record iliyopo Tabata jijini, Chini Sheddy akiwa amekaa katika gari.
MTAYARISHAJI MWENYE NDOTO ZA KUFANIKIWA, MAN WATER ALIMVUTA KWENYE GEMU, SASA ANAWANIA TUZO ZA KILL MUSIC AWARD


ANAJULIKANA kwa jina la Sheddy Clever lakini familia yake inamfahamu kwa jina la Shadrack Moigi kijana mdogo ambaye amejikita kwenye tasnia ya utayarishaji muziki maarufu kama prodyuza.

Sheddy Clever ama Sheddy (Pichani) ukienda mitaa ya Tabata utakutana naye ni miongoni mwa watayarishaji chipukizi waliopiga hatua kubwa kimuziki, Akielezea kuanza kwake kazi hiyo ya uprodyuza.

Sheddy amesema kuwa alianza kazi hiyo mwaka 2008 mkoani Tabora na amemtaja prodyuza Man Water kuwa ndiye aliyemfanya aingie kwenye tasnia hiyo ya utayarishaji.

'Nilivutiwa sana na kazi zake na ndio maana nikaamua kujitumbukiza mara baada ya kumaliza masomo', alisema na kuongeza, 'mimi nilikuwa Dj katika ukumbi wa disco Muungano Masse huko huko Tabora nikiwa nasoma', alisema.

'Mwaka 2009 nilihamia jijini Dar es Salaam ambaposasa nilikua kikazi zaidi, nilikutana na wasanii mbalimbali wakubwa na wadogo nikafanya nao kazi, Na kazi yangu ya kwanza ilikuwa ya PNC na Ney Wa Mitego iitwayo 'Swaga'aliongeza.

Anasema kuwa wimbo wa Swaga ndio ulioanza kumtoa na kumfanya aanze kusikika katika ramani ya muziki, 'Baadaye nikakutana na Dayna tukafanya 'Nivute Kwako' ndipo mashabiki wakazidi kunielewa', alisema Sheddy.

Aliongeza kuwa kuwa aliendelea kufanya kazi nyingi zaidi na wasanii mbalimbali ukiwemo wimbo wa 'Marry Me' wa Rich Mavoko, Zilipendwa wa Matonya na nyinginezo.

Kwa sasa Sheddy ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za Kilimanjaro Music Award hivyo anahitaji sapota ya mashabiki ili aweze kushinda tuzo hizo ambapo yeye anawania utayarishaji bora chipukizi wa mwaka jana.

Sheddy ametoa maelekezo ya kumwezesja kuwa mshindi ambapo amesema kuwa jinsi ya kumpigia kura andika neno  BF5 kwenda namba 15345 na itamwezesha kuibuka mshindi katika tuzo hizo.

Kwa sasa Sheddy anamiliki studio yake binafsi ya Burn Record iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa studio yake imetoa punguzo la bei kwa wasanii chipukizi.

Akizungumza na mambouwanjani.blogspot.com Sheddy amesema kuwa ameamua kupunguza bei kwa wasanii wachanga ili kukuza na kuendeleza muziki hapa nchini, Sheddy alizaliwa mkoani Tabora na kusoma katika shule ya msingi ya Isike iliyopo Tabora ambapo alimaliza elimu ya sekondari katika shule ya Ally Hassan Mwinyim Huyo ndiye Sheddy Clever

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA