Kura Tuzo za Kili mwisho Ijumaa
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe
Tamasha la kukabidhi tuzo hizo litafanyika Juni 8 mwaka huu ambapo tuzo 37 zitatolewa.
Akizungumza jana jijini, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema kuwa kampuni inayosimamia kura hizo itafunga zoezi hilo Ijumaa usiku na haitahesabu kura zitakazopigwa baada ya muda huo uliopangwa kumalizika.
Kavishe alisema kuwa wanafurahishwa na hamasa iliyojitokeza mwaka huu ambapo hadi juzi, taarifa walizonazo ni kwamba idadi ya kura zilizopigwa ni mara mbili ya zile zilizopigwa mwaka jana wakati wa mchakato huo wa kusaka washindi.