KIIZA AITOSA YANGA, AIFUATA SIMBA KINESI
Hamis Kiiza
Kiiza ameutaka uongozi wa Yanga umpe Dola za Marekani 50,000 (Sh. milioni 80) kwa ajili ya kusaini mkataba mpya na pia umpe mshahara wa Dola za Marekani 3,000 (Sh. milioni 4.8) kila mwezi.
Kiongozi mmoja wa juu wa Yanga (jina tunalihifadhi) alisema kuwa endapo Kiiza ataendelea kuwa na msimamo huo, nafasi yake itachukuliwa kiulaini na kipa Mghana, Yaw Berko na kiungo Mnyarwanda, Kabange Twite.
"Licha ya mazungumzo na kumweleza msimamo wetu, alibaki na msimamo wake na hadi alipoamua kwenda kwao, alituandikia barua akieleza kwamba atakuwa tayari kusajili kwa Dola za Marekani 45,000 na si chini ya hapo,".
Kiongozi huyo aliongeza kuwa Kiiza anatakiwa akubali kushusha kiwango cha fedha cha usajili ili asajiliwe la sivyo nafasi yake itachukuliwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb, aliliambia gazeti hili kuwa kamati yake bado iko katika mazungumzo na wachezaji hao watatu na itakapofikia mwisho itawasajili wawili.
Binkleb alisema kwamba kamati yake inafanya maamuzi ya kumsajili mchezaji baada ya kuridhishwa na kiwango cha mchezaji husika na kuridhiwa na vipengele vitakavyokuwapo ndani ya mkataba.
Alisema pia wanataka kumaliza zoezi la usajili wiki hii ili mapema wiki ijayo programu ya mazoezi ya timu yao ianze kwa ajili mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo ambayo mwaka huu yatafanyika kuanzia Juni 18 hadi Julai 2 huko Sudan.
Kuna taharifa zinasemekana kuwa Kiiza anajiandaa kuwasili nchini lakini ataifuata klabu ya Simba ambayo imemunyeshea nia ya kumsajili, Kiiza alianza mazungumzo na viongozi wa Simba kabla mkataba wake haujamalizika