Kiemba aikana Yanga, Kumwaga wino Msimbazi
Na Elias John
KIUNGO wa kutegemewa wa klabu ya Simba Amri Kiemba ameikana klabu ya Yanga na kudai yeye atasaini tena katika timu yake ya Simba licha ya mkataba wake kumalizika.
Kiemba alihusishwa kutua Yanga lakini amekataa uvumi huo na kuwataka Wanasimba kutulia katika kipindi hiki cha usajili kwani kuna mengi yatazushwa.
'Licha ya mkataba wangu kumalizika bado nitaongeza mkataba mwingine na mipango yote imeshakamilika, Hata mimi nilikuwa nikizisikia taharifa hizo lakini nawatoa wasiwasi sina mpango wa kwenda Yanga', alisema Kiemba ambaye yuko kwenyekikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kurudiana na Morocco.
Yanga imeonekana kufanya usajili wa nguvu kujiandaa na msimu ujao ambapo itashiriki ligi ya mabingwa Afrika, Tayari mabingwa hao wa bara na Afrika mashariki na kati wameshamalizana na mshambuliaji wa Azam Mrisho Ngassa ambaye alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo.