Kibaden aanza kazi leo,achimba mkwara kwa Julio

Na Mwandishi Wetu

KOCHA mpya wa Simba Abdallah Kibaden Mputa (Pichani) ambaye amemaliza mkataba wake na timu ya Kagera Sugar  ameonyesha kumpiga mkwara mzito kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelo 'Julio', Kibaden ambaye leo ameanza kazi ya kuinoa Simba katika uwanja wa Kinesi alitoa mkwara kwa Julio hivi karibuni
.

Akizungumza katika kipindi cha michezo kinachotangazwa na redio Magic Fm hivi karibuni , Kibaden aliyetua Simba kwa makataba wa miaka miwili na  kurithi mikoba ya Mfaransa Patrick Liewig ambaye amerejea nchini kwao kwa mapumziko ameonyesha kutomuogopa Julio na kudai ni sawa na mwanaye wa kumzaa.

Kibaden anasema kuwa Julio ni kijana wake na alikutana naye Simba mara mbili, Mara ya kwanza akiwa anaifundisha Simba ambapo Julio alikuwa mchezaji, Na mara ya pili alikutana naye kama msaidizi wake ambapo yeye alikuwa kocha mkuu na Julio msaidizi.

Hivyo Kibaden amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Julio endapo Simba watamalizana naye kama kocha mkuu wa kikosi hicho kilichopokwa ubingwa wa ligi kuu ya bara na hasimu wake Yanga, Hata hivyo Kibaden amemalizana na Simba na sasa anainoa timu hiyo.

Kibaden alipigiwa chapuo kuchukua nafasi ya Liewig ambaye inasemekana anaweza kutoswa, Liewig ameiongoza Simba kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu huku akitumia kikosi cha vijana yaani B.

Kwa kumchukua  Kibaden Simba itakuwa imeondokana na makocha wa kigeni kwani ilikumbwa na misukosuko mikubwa msimu huu hasa kudaiwa fedha na makocha wake wa kigeni ambao hulipwa mishahara mikubwa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA