JAYDEE AZIDI KUJIKAANGA MWENYEWE

Nyota wa muziki wa Bongofleva,Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee
 
Nyota wa muziki wa Bongofleva,Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee, amesema kwamba aliyoyaandika katika waraka alioutuma kwenye blogu yake kwamba viongozi wa Clouds Group "wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaomuingizia chochote unakatika", ni ya kweli na aliyaandika kwa nia njema.


Jaydee ameeleza hayo katika utetezi wake aliouwasilisha jana kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kujibu tuhuma zinazomkabili katika kesi ya madai dhidi yake iliyofunguliwa na viongozi wa Clouds Mei 14, mwaka huu.

Katika hati ya madai, Clouds Group wanaiomba mahakama imuamuru msanii huyo awaombe radhi hadharani katika chombo kinachoheshimika kwa kuwachafua katika jamii, imzuie Jaydee na wadau wake kutoa kauli za kuwachafua walalamikaji, izuie taarifa zote alizotoa kwa kuzichapisha ama kurekodi ili zisiendelee kusikika/kufikiwa na yeyote, alipie gharama zote za kesi hiyo na pia alipie hasara ya jumla waliyopata walalamikaji kulingana na itakavyokadiriwa na mahakama.

Jaydee aliwasilisha hoja zake mahakamani hapo jana saa 2 asubuhi akiwa amefuatana na mume wake Gadner Habash na wakili wake, Gabliel Mnyele.

Hata hivyo, walalamikaji nao wameiomba mahakama kujibu hoja zilizowasilishwa na Jaydee na watawasalisha hoja zao mahakamani hapo Juni 3 mwaka huu. Kesi hiyo itasikilizwa kwa hakimu Athumani Nyamlani Juni 13, mwaka huu saa 5 asubuhi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA