HATIMAYE JOSE MOURINHO ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE KUJIUNGA TENA NA CHELSEA
JOSE MOURINHO ni boss mpya wa Chelsea — na hiyo ni rasmi kwa mujibu wa gazeti la The Sun!
The Special One ameripotiwa kusaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya £40million jana usiku.Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa juu wa Chelsea: “Ni rasmi Jose ni kocha wetu tena! Kila mtu anafurahia ujio wake - klabu, wachezaji na mashabiki.
“Tayari tunajiaandaa na msimu ujao - tuna uhakika utakuwa msimu mzuri sana.”
Mechi ya kwanza ya Mourinho inatarajiwa kuwa kwenye mechi ya mataarisho nchini Thailand dhidi ya Singha All Stars XI, katika ziara ya huko Malaysia na Indonesia.
Baada ya hapo The Blues wataenda Marekani kwenye michuano ya International Champions Cup itakayohusisha timu za Real Madrid na Inter Milan, pia Everton, Juventus, AC Milan, Valencia na LA Galaxy.