CLOUDS KUGHARAMIA KULETA MWILI WA NGWEA DAR KESHO

Baada ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika
 katika hospitali ya Hillbrow, mwili wa marehemu Albert
 Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili Jumamosi kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini,
ukitokea nchini Afrika ya kusini.

 Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali
 ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, ni
 kwa hisani ya Clouds
Media Group. Ndio waliogharimia safari ya
mwili wa marehemu.


 Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert
 Mangwea utakuwa unaagwa viwanja vya leaders
club na kampuni
itakayoshughulikia
zoezi hili ni Entertainment Masters na baada
 ya mwili kuagwa,
safari ya kumsindikiza Albert Mangwea
kuelekea kwenye maziko
 itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro.




Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la
 Kihonda, mkoani,
Morogoro...!!

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA