BREKING NEWS: MOSES OLOYA KUTUA SIMBA

KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Moses Oloya (20) yupo katika mazungumzo na na klabu ya Simba SC, ambayo yanaendelea vizuri.


Tayari mshambuliaji huyo wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam amerejea Kampala, Uganda kujiunga na timu yake ya taifa, kwa ajili ya mechi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia.

Kiongozi wa Simba SC yupo Uganda tayari na anaendelea na mazungumzo na kiungo huyo, ambaye aling’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwishoni mwa mwaka jana na kuiwezesha Uganda kutwaa Kombe.

Kiongozi huyo aliyefanikisha usajili wa Mganda mwingine, beki Samuel Ssenkoom wa URA, amefikia sehemu nzuri katika mazungumzo na mchezaji huyo mwenye nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. 
Bila shaka, kama mazungumzo yataendelea vizuri, ndani ya siku mbili Oloya atasaini Simba SC.

Na ikimpata mchezaji huyo aliyezaliwa Oktoba 22, mwaka 1992, akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010, Simba itakuwa imelamba dume.
Oloya ni mchezaji mzuri kuliko Emmanuel Okwi ambaye Simba SC imemuuza Etoile du Sahel ya Tunisia na Desemba mwaka jana, Yanga SC na Azam zote zilijaribu kutaka kumsajili bila mafanikio.

Mwishowe Azam ikaona bora kumsajili Brian Umony, wakati Yanga ilibanwa na nafasi ya idadi ya wachezaji wa kigeni, lakini ikamuweka kwenye orodha ya wachezaji inayoweza kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA