ARSENAL HATARINI KUIKOSA LULU YA SERIE A
MPANGO wa Arsenal kumsajili Stevan Jovetic uko hatarini kubuma kwa sababu zile zile mashuhuri za klabu hiyo ya London, 'ubakhili uliotukuka'.
Arsenal imeshindwa kutoa dau la Pauni Milioni 25 ambalo Fiorentina wanataka ili kumtoa Jovetic.
Mazungumzo
baina ya klabu hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa sasa,
baada ya kocha Arsene Wenger kumfanya Jovetic mchezaji nambari moja
katika orodha ya nyota anaowataka kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
Lakini
mpango huo unaelekea kubuma, kutokana na klabu hiyo ya Serie A kugoma
kuchukua kiasi chochote cha fedha chini ya Pauni Milioni 25 walizotaka.
Ubakhili
utawakosesha kifaa hiki: Mchezaji anayetakiwa kwa muda mrefu Arsenal,
Stevan Jovetic wa Fiorentina anauzwa Pauni Milioni 25
Mabosi
wa Gunners, wameiambia Fiorentina wako tayari kulipa tu Pauni Milioni
20 ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Montenegro na kuna wasiwasi Juventus nao wanamnyatia Jovetic.
Kama
Arsenal, vigogo hao Italia nao wameanzisha mazungumzo na klabu yake juu
ya kumsajili Jovetic — lakini inafahamika itakuwa jambo gumu kwa
Fiorentina kuwauzia silaha wapinzani wake.
Andondoka: Andrey Arshavin (kushoto), akiwa mazoezini na Jack Wilshere, anaweza kutimkia Zenit St Petersburg
Pamoja na hayo, Juventus wako tayari kutoa dau ambalo Fiorentina wanataka, ili kuwabadilisha mawazo yao.
Wakati huo huo, Andrey Arshavin, ambaye amemaliza mkataba wake, anatakiwa na Zenit St Petersburg.
Mshika
Bunduki huyo 'aliyetepeta', ambaye analipwa Pauni 90,000 kwa wiki, pia
ana za kwenda kucheza Marekani na Mashariki ya Kati.