AFYA NA JAMII
SABABU ZA MDOMO KUNUKA NA MENO KUOZA
Na Mwandishi Wetu
LIMEKUWA tatizo kubwa kwa binadamu wa aina zote wakubwa kwa watoto kusumbuliwa na maradhi ya meno ambapo sasa tatizo hili limezidi kupita kiwango.
Zamani ilikuwa imezoeleka watu wenye umri mkubwa hasa wazee walikuwa wakisumbuliwa na maradhi ya meno na kusababisha mdomo kutoa harufu kali inayotia kinyaa.
Lakini kwa miaka hii ya sasa matatizo ya meno kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 15-25 limezidi kuwa kero na kuwasababishia vijana hao kukosa raha kutokana na kuoza kwa meno yao na kutoa harufu mbaya.
Mkurugenzi wa kituo cha utafiti na tiba mbadala Dk Ndulumo amezungumzia maradhi ya meno na dalili zake huku akitoa tahadhali jamii kutopendelea kula vyakula fulani.
Dk Ndulumo ambaye ni mmiliki wa kituo chake cha tiba mbadala kijulikanacho Goligota Herbs, ameiambia MAMBO UWANJANI kuwa maradhi ya meno husababishwa na ulaji wa vitu vitamu pamoja na kutopendelea kusafisha meno kwa wakati.
Amesema kinywa cha binadamu kina bakteria wengi waliojificha ambao hushambulia mabaki ya chakula yanayosalia kwenye meno, Bakteria hao hula mabaki hayo na kuzishambulia fizi ambapo baadaye hukimbilia kwenye meno ya kuyala.
Meno huoza na kusababisha maumivu makali toka kwa kuathilika, Dk Ndulumo anasema, 'Kula vyakula vya moto sana, kutokupiga mswaki kikamilifu na kwa wakati hupelekea tatizo la kuoza kwa meno', alisema.
Aidha aliongeza kuwa kwa kawaida mswaki hutakiwa kutumiwa mara tatu kwa siku, Matumizi mabaya ya vyakula vyenye sukari nyingi mfani pipi na biskuti, alisema.
Alizitaja sababu nyingine zinazopelekea kuharibika kwa meno, 'Sabau za kimaumbile yaani kurithi, Matumizi kinyume ya meno mfano kufungulia kinywaji kama soda, maji na bia kwa kutumia meno', aliongeza.
'Kutafuna meno yenyewe nk, Tiba yake ipo, kwa upande wa tiba mbadala kuna dawa za uhakika ambazo mgonjwa huzitumia kwa kuweka kwenye mswaki kusukutua na kung'atia', alieleza.
Ili kuonana na Dk Ndulumo unaweza kumpigia simu kwa kutumia namba yake ya kiganjani 0713 690868 au fika katika kliniki yake iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam