YANGA YAITOSA SIMBA, KULA PILAU NA COASTAL UNION KESHO

30/05/2013

Na Prince Hoza

KAULI iiliyotolewa jana na mmoja kati ya wajumbe wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb imedhihirisha kuwa Yanga imeitosa mechi yao dhidi ya Simba ambayo ilipangwa kula pilau lao la ubingwa wa bara.

Bin Kleb aliyasema hayo jana wakati akizungumza nna kituo cha redio cha Magic Fm kupitia kipindi cha michezo, Mjumbe huyo alisema kuwa kesho watakula pilau lao la ubingwa itakapocheza na Coastal Union ya Tanga kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga iliapanga kusherehekea ubingwa wake wa bara ilioutwaa bila jasho Mei 18 itakapokutana na mtani wake wa jadi Simba SC, Lakini imeamua kusherehekea kesho itakapomenyana na Coastal Union ya Tanga ambao waliitengenezea njia Yanga ya kutwaa ubingwa huo siku ya Jumamosi ilipotoka sare na Azam Fc ya 1-1.
Yanga kesho inacheza mchezo wake wa 23 ikiwa tayari imeshatangazwa kuwa mabingwa wa bara na kuivua Simba ubingwa huo iliyokuwa ikiushikilia, Aidha Bin Kleb alisema kuwa Simba si mpinzani wa Yanga mwaka huu na mpinzani wao ni Azam ambao wameshika nafasi ya pili.
Hivyo mechi yao wanakwenda kukamilisha ratiba tu na wanaifananisha na mechi nyingine walizocheza na timu kama za Mgambo Shooting au JKT Oljoro.
'Simba hawatishi kwanza msimu huu si wapinzani wetu, Ni hasimu tu ila mpinzani wetu ni yule aliyeshika nafasi ya pili ambao ni Azam', alisema Bin Kleb, 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA