SIMBA YAWAVUA MAGWANDA POLISI MORO
![](https://fbcdn-sphotos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/542523_341606939258906_546257723_n.jpg)
MABINGWA wa zamani wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba SC jana waliwavua magwanda Polisi Moro baada ya kuifunga magoli 2-1 kwenye uwanja wa Taifa jijini, Polisi Moro ambayo ilistahili ushindi mechi hiyo ili ijiwekee mazingira ya kubaki ligi kuu lakini ilijikuta inashindwa kuhimili mashambuliizi ya wachezaji wa Simba.
Kwa matokeo hayo sasa Polisi inasubiri miujiza tu ili kubaki ligi kuu, magoli ya Simba yalifungwa na Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa, Hata hivyo Simba inajiandaa vilivyo kabla haijakutana na hasimu wake mkubwa Yanga Mei 18