SHEDY CLEVER AOMBA SAPOTA KWA MASHABIKI WAKE
30/05/2013
MTAYARISHAJI anayeibukia katika kutengenza nyimbo za muziki wa kizazi kipya hapa nchini Shedrack Moigi ama Shedy Clever wa studio ya Burn Record iliyopo Tabata amewaomba mashabiki wake kumpa sapoti.
Shedy (Pichani kushoto) ambaye ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo zinazotolewa na Kill Music Award zitakazofanyika mwaka huu amesema kuwa anawapenda sana mashabiki wake hivyo anaomba wampigie kura na aibuke mshindi.
Akizungumza na mambouwanjani.blogspot.com amedai kuwa anawashukuru Watanzania kwa ushirikiano wao kwake na kukubali kazi zake.
Aidha amesema kuwa Watanzania wamemwelewa kutokana na kazi zake hivyo hatowaangusha, 'Nikweli Watanzania wamenikubali na wanajua kitu gani nafanya hivyo nitaendeleza yale ninayoyafanya sasa' alisema.
Ameongeza kuwa atakuwa bega kwa bega na wala kuwaangusha watu wake, Mtayarishaji huyo amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kufanikiwa kutengeneza nyimbo zinazofanya vizuri sasa na kumfanya aingine kwenye kuwania tuzo hizo kubwa kabisa hapa nchini.
Shedy anawaomba Watanzania kura ili aibuke mshindi, Mtayarishaji huyo anawania tuzo ya mtayarishaji bora anayechipukia, Kazi zake zilimfikisha hapo ni pamoja na wimbo wa 'Merry Me' wa Rich Mavoko, 'Amekua' ya Pasha na Tundaman, 'Zilipendwa' ya Matonya, 'yatakwisha' ya Ben Poul na Linnah ambazo alizitengeneza mwaka 2012.
Amemalizia kwa kusema anawaomba sana ushirikiano Watanzania ili achukue tuzo hiyo