Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2024

Ramovic amtosa Makame Yanga

Kocha Sead Ramovic ameukataa usajili wa mlinzi wa kati wa Fountain Gate FC, Laurian Makame baada ya kumtazama kwenye mchezo kati ya Fountain Gate FC dhidi ya Azam FC. Uongozi wa Yanga ulikuwa ushafanya kila kitu ili Laurian Makame ajiunge na Yanga ila imeshindikana baada ya Ramovic kumkataa, Kama mwalimu angekubali usajili wake basi mchezo wa jana asingekuwa sehemu ya kikosi cha Fountain Gate FC bali angekuwa ndani ya Yanga. Dili lake lilikuwa asilimia 90% linakwenda kukamilika.

Chasambi kupoteza ushirikiano kwa nyota wenzake Simba

Kiungo mkabaji wa Yanga SC Khalid Aucho ameoneshwa kumsikitikia kiungo mshambuliaji kinda wa Simba Ladack Chasambi kwamba kww kauli aliyoitoa ambayo imekuqa gumzo. Chasambi bado ni kijana mdogo ana safari ndefu ya kujifunza lakini kwa kauli kama ile ni rahisi kupoteza ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzake, lakini pia nawashangaa wachezaji wa hapa Tanzania wana vipaji vikubwa sana ila hawaheshimiani. “Mchezaji kama Feitoto kafanya makubwa kwa misimu zaidi ya mitatu sasa ulitegemea mchezaji kama Chasambi ajifunze mengi kwake"

Tabia Batamwanya amlilia Sunday Mwakanosya

Mwanamuziki wa dansi Tabia Batamwanya ameguswa na kifo cha aliyekuwa mtangazajj wa Magic Fm, Sunday Mwakanosya kilichotokea jana katika hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila. Akizungumza kupitia kurasa yake ya Facebook, Batamwanya ameguswa na msiba huo akidai ni pigo kubwa kwa muziki wa dansi kwani marehemu alikuwa na mchango mkubwa. "Namfahamu kwa muda mrefu marehemu Sunday, sina la kusema zaidi ya kumtakia mapumziko mema peponi Amina" alisema Batamwanya ambaye ni mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa dansi Tabia Batamwanya (kushoto)

Karabaka atimkia Namungo FC

Kiungo mshambuliaji Wa Klabu ya Simba Saleh Karabaka amejiunga na klabu ya Namungo kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita hadi mwishoni mwa Msimu huu. Karabaka alijiunga na Simba Januari mwaka huu kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Klabu ya JKU ya Visiwani Zanzibar. Saleh Karabaka

Kilimanjaro Stars waenda Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars leo wamesafiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi itakafanyika uwanja wa Gombani, Zanzibar. Mapema leo wachezaji hao na benchi lake la ufundi chini ya Ahmad Ally, wakiwa bandarini walianza safari kuzifuata timu nyingine za taifa kushiriki michuano hiyo mipya.

Kocha wa makipa Geita Gold afungiwa kisa kushika nyeti za mwamuzi

Kocha wa Makipa wa Geita Gold, Augustino Malindi, amefungiwa mechi 16 pamoja na faini ya Milioni 1 kwa kosa la kumshika sehemu za siri mwamuzi wa akiba katika mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Geita Gold. Baada ya kuonywa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi namba moja (1) wa mchezo huo. Kocha huyo alitenda kosa lingine akiwa anakwenda vyumbani baada ya kuonywa kwa kadi nyekundu, kwa kumshika kifuani mratibu wa mchezo huo ambaye ni mwanamke jambo ambalo ni kinyume na maadili ya ukocha na mpira wa miguu kwa ujumla. Pia amefungiwa mechi 3 na faini 500,000 kwa kumtukana Ass Ref 1.

Kilimanjaro Stars kamili kushiriki kombe la Mapinduzi

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars, Ahmad Ally ametangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano mipya ya kombe la Mapinduzi itakayofanyika katika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar. Mbali ya kuita nyota wapya, baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakiitwa mara kwa mara kwenye timu ya taifa ya Taifa Stars wamejumuhishwa pia.

Sunday Mwakanosya afariki dunia

Mtangazaji wa kituo cha redio cha Magic Fm, Sunday Mwakanosya amefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema Mwakanosya amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi. Enzi za uhai wake Mwakanosya alikuwa akitangaza kipindi cha muziki wa dansi na alikuwa mdau mkubwa wa muziki huo. Mungu aipumzishe roho yake mahara pema peponi.

Tanzania Prisons yapata kocha mpya

Rasmi Tanzania Prisons imefanikiwa kuinasa Saini ya Kocha Wa Geita Gold inayoshiriki Championship Josia Amani. Josia anachukua mikoba ya Mbwana Makata ambae ameondoka Tanzania Prisons. Josia Amani akiwa Geita Gold FC amecheza michezo 14, amekusanya alama 30 anashika nafasi ya pili nyuma ya Mtibwa Sugar.

Yanga yarudia kuua 5G

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC imekuwa ya moto zaidi baada ya kuilaza Fountain Gate mabao 5-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam. Pacome Zouzoua dakika ya 15 alifungua akaunti ya mabao kabla ya Mudathir Yahya dakika ya 40 kufunga bao la pili, moto wa Yanga uliendelea tena pale Zouzoua alipofunga bao lake la pili kwa mchezo wa leo na la tatu kwa Yanga dakika ya 45. Mabingwa hao wa bara waliandika bao la nne dakika ya 51 kupitia kwa Jackson Shiga aliyejifunga, Clement Mzize dakika ya 87 alifunga bao la tano na la sita kwake. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 39 nyuma ya Simba yenye pointi 40 zikifukuzana kileleni

AmaZulu kumng'a Kibu Msimbazi

Klabu ya AmaZulu ya Ligi Kuu ya Soka Afrika Kusini imetuma ofa kumsajili Mshambuliaji wa Simba SC ya ligi kuu Tanzania Bara, Kibu Denis (26). AmaZulu imefanya mazungumzo na Wekundu wa Msimbazi kuhusu Kibu, AmaZulu FC iliyochini ya kocha Pablo Franco Martin aliyewahi kuwa kocha wa Simba SC tangu 2021 - 2022, AmaZulu katika msimu huu wa ligi kuu soka Afrika Kusini inashika nafasi ya 13 kwa alama 9 ilizovuna kwenye michezo 9. Msimu uliopita ilifanikiwa kumaliza nafasi ya 11 kwenye ligi kuu ikiwa na alama 36 katika michezo 30.

TMA Stars yang' oa mmoja Kagera Sugar

Klabu ya TMA Stars ipo kwenye mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar na Mwadui Venance Ludovick. Msimu huu Ludovick amewatumikia wapiga debe kutoka pale Shinyanga Stand United.

Gamondi kuwa kocha mkuu Raja Casablanca

Aliyekuwa kocha wa Yanga Sc, Miguel Angel Gamondi yupo ukingoni kutangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Raja Casablanca ya Morocco akichukua mikoba ya Ricardo Sa Pinto aliyetupiwa virago wiki iliyopita. Gamondi raia wa Argentina anatarajiwa kuwa kocha wa tatu kuinoa Raja AC kama kocha mkuu msimu huu baada ya Ricardo Sa Pinto na Rusmir Cviko. Cviko alichukua mikoba ya Josef Zinnbauer aliyeinoa klabu hiyo akisaidiwa na Fadlu Davids wa Simba Sc kwa mafanikio msimu uliopita huku klabu hiyo ikimaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote.

Mchezaji wa Chelsea mbioni kutua Simba

Kiungo mshambuliaji raia wa Ghana na klabu ya Berekum Chelsea Stephen Amankona yupo katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Simba Sc katika dirisha hili dogo la usajili Amankona anatarajia kuanza safari kuja nchini Tanzania kumalizia sehemu ya makubaliano yaliyosalia ili kukamilisha dili hilo la kujiunga na Simba Kiungo mpaka sasa kwenye klabu yake kafanikiwa kufunga magoli 5 katika michezo 12 aliyocheza Hana Assisti

Diana Mnally asaini Yanga Princess

YANGA Princess imekamilisha uhamisho wa mlinzi wa kushoto Diana Mnally kutoka Gates Program. - Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa imani yao ni kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Simba Queens atakuwa sehemu ya mafanikio yao. - Msimu uliopita Diana aliachana na Simba Queens na kujiunga Gates Program lakini sasa amepata malisho mapya huko jangwani. - Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya wanawake anaingia katika orodha wa wachezaji wa kike waliokipiga Simba na Yanga, wengine ni Amina Ally, Precious Christopher, Saiki Atinuke, Danai Bobo,Wema, Daniella Ngoyi nk.

Chilunda kurejea uwanjani na KMC

Shabani Iddy Chilunda yupo majaribio kwenye klabu ya KMC FC akitafuta nafasi ya kusajiliwa baada ya kukaa nje ya uwanja takribani miezi mitano (6) baada ya mkataba wake na Simba SC kumalizika. Ni pendekezo la Mwalimu Ongala ambaye alifanya nae kazi Azam FC uongozi umempa nafasi ya kujaribu bahati yake kwenye majaribio kabla ya kumsajili moja kwa moja.

Bui atemwa Zanzibar Heroes

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman Moroco amemuondoa kwenye timu Mchezaji Abdulaziz Makame "Bui" wa Geita Gold FC kwa makosa ya utovu wa nidhamu pamoja na kutokufika Kambini kwa wakati, huku akiwa amesharuhusiwa na timu yake kwa muda mrefu. Moroco amewaongeza kwenye timu, Abubakar Nizal kutoka Azam FC U20 na Abdulnasir Mohamed Abdallah 'Casemiro' Mlandege FC

Kutoka Yanga hadi KVZ

Klabu ya Soka ya KVZ FC imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji nyota raia wa Tanzania Yohana Mkomola (24) na kumsainisha mkataba wa Miaka 2 kuhudumu ndani ya klabu yao. Ikumbukwe Yohana ambaye alishawahi kuhudumu katika kikosi cha Tabora United ni miongoni mwa wale Nyota kizazi cha Dhahabu cha wakina Dickson Job, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage na Wakina Ramadhani Kabwili. Pia aliwahi kuichezea Yanga SC kabla ya kutimkia Ukraine. Akiwa FIT Mkomola ni miongoni mwa Vipaji hatari sana na wanauwezo mkubwa sana wa kuiweka safu ya timu pinzani matatani, naamini hapa KVZ wamepata mtu haswa na atawasaidia.

Simba yaitambia Singida Black Stars nyumbani kwao

Timu ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye uwanja wa Liti mjini Singida mchezo wa Ligi Kuu bara. Kwa ushindi huo sasa Simba imefikisha pointi 40 na mechi 15 na kukaa kileleni huku ligi ikienda kusimama kupisha brecking, bao pekee la Simba limefungwa na Fabrice Ngoma dakika ya 42. Kesho watani zao Yanga SC watawaalika Fountain Gate katika uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam, Yanga hata kama ikiehinda haitaweza kuifikia Simba.

Ramovic amfunika Gamondi

Kocha mkuu wa Yanga Saed Ramovic amekuwa na takwimu bora sana tangia ajiunge na Yanag tofauti na mtangulizi wake Miguel Gamondi. Hadi hivi sasa Ramovic ameiongoza Yanga kwenye michezo minne ya Ligi, timu yake imefunga magoli 13 imefungwa magoli mawili tu . Miguel Gamondi ameiongoza Yanga kwenye michezo kumi msimu huu , timu yake imefunga magoli 14 na kufungwa magoli manne .

Azam FC yaikung' uta JKT Tanzania 3-1

Kikosi cha Wanalambalamba Azam FC usiku huu wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu bara. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Paschal Msindo na Iddi Nado aliyefunga mabao mawili, bao pekee la kufuta machozi la JKT Tanzania lilifungwa na Juma. Kwa ushindi huo Azam FC imefikisha pointi 36 ikilingana na Yanga yenye pointi 36.

KenGold yanasa Mghana wa Pamba Jiji

Klabu ya KenGold Imekamilisha Usajili wa Mkopo wa Miezi Sita wa aliyekuwa Mshambuliaji wa klabu ya Pamba Jiji Eric Okutu (31) ambaye ni Raia wa Ghana, Okutu anatarajia kujiunga na klab ya KenGold baada ya klabu yake ya Pamba Jiji FC kumaliza mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons. Okutu kabla ya kujiunga na klab ya Pamba Jiji alikuwa akiitumikia klabu ya Tabora United.

Ramovic hataki ukae na mpira- Pacome

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Pacome Zouzoua ameweka wazi kuwa kocha Saed Ramovic ni mkali sana hataki kabisa mchezaji akae na mpira kwa muda mrefu akiwa uwanjani. “Kocha ni mkali sana.Hataki ukae na mpira mguuni muda mrefu.Anataka twende mbele kwa kasi yaani gusa tuondoke.Tumeona mabadiliko makubwa sana.Mbinu zake na mifumo yake inataka uwe na pumzi ya kutosha." "Hataki kuona kabisa unakaa na mpira hata sekunde tano.Ukiupata unatakiwa kujua unaupeleka wapi na kwenda kuunda umbo wapi.Kifupi tukabe wote, tufunge wote.“ Pacome Zouzoua, kiungo wa klabu ya Yanga.

Joshua Mutale kurudi Power Dynamo

Simba SC itamtoa Kwa Mkopo Winga wao Joshua Mutale kabla Dirisha la Usajili Kufungwa. Inaelezwa kuwa Timu yake ya Zamani Power Daynoms Iko tayari kumrejesha Nyota Huyo Mpka mwisho Wa Msimu huu.

Kushuka kiwango kumemuondoa Namungo, Djuma Shabani

BAADA ya kuitumikia Namungo kwa muda wa miezi sita kabla ya kutangazwa kutemwa, beki wa zamani wa AS Vita na Yanga, Djuma Shaban amefunguka sababu za kuvunja mkataba na Wauaji wa Kusini hao akisema ni kushindwa kutumika mara kwa mara kikosini. “Tangu nimejiunga na Namungo sina mwendelezo mzuri wa kucheza, hiyo haikuwa afya kwangu na kwa timu kwa vile walinisajili ili nicheze, naamini katika upambanaji na kucheza,” “Nimeamua kujipumzisha kwa muda ili kujiweka kwenye utimamu mzuri nitarudi tena kucheza nikiwa imara na nitacheza kwa mafanikio.” “Nimecheza misimu miwili nikiwa na Yanga sasa nimemalizana na Namungo kuna utofauti mkubwa nimeuona, kuna mabadiliko ya timu na timu pia kuongezeka kwa wachezaji wa kigeni kwa timu tofauti,” - Amesema Djuma Shaban

Mchanja Yohana amchanja Mphilipino

TAIFA la Tanzania bado lipo kwenye mikono salama usiku huu baada ya Bondia Mtanzania Mchanja Yohana kutembeza kichapo usiku wa jana kwa kumchapa makonde ya kutosha bondia kutoka Philipino Miel Fajardo na kushinda kwa pointi 116 kwa 111 za majaji wote watatu. Pambano hilo la raundi 12 kwenye pambano la Knock out ya Mama ndani ya ukumbi wa Super Dome hapa Masaki na kufanikiwa kushinda mkanda wa World Boxing Organization Global flyweight championship (WBO Global). Kwa ushindi huo wa pointi, Mchanja anaondoka na kitita cha KnockoutYaMama cha Sh milioni tano (5 Milioni).

Hussein Massanza aibeza Simba na kuwaita akademia

Msemaji wa timu ya Singida Black Stars ya mkoani Singida, Hussein Massanza ni kama amewabeza Simba SC kwa kudai kwamba imesajili wachezaji vijana hivyo ni akademia. Msemaji huyo amedai kwamba katika mchezo wao wa kesho katika uwanja wa Liti, Simba SC wasitegemee kubebwa kwa kupewa penalti isipokuwa watafungwa zaidi ya goli moja kwakuwa wanao wachezaji wazuri wa kumaliza mechi. 'Nawaona Simba SC kama academy kwa sababu wamekusanya vijana wengi wadogo wadogo kama wapo kwenye majaribio" Simba SC ni timu yenye mipango hata sisi tunaijua na tutapita humo humo kwa sababu mechi tunaitaka" Alisema Hussein_Massanza Msemaji wa klabu ya Singida Black Stars. Hussein Massanza

Nabi akalia kuti kavu Kaizer Chief

Kocha wa Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi, aliyewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio makubwa. Nabi anakabiliwa na shinikizo kubwa la kurejesha heshima ya timu hiyo, kwani ikiwa nafasi ya tisa kwenye ligi ya Afrika Kusini inaashiria huu ni msimu mwingine uliojaa matokeo yasiyoridhisha. Mashabiki wa Amakhosi wanaanza kutilia shaka kama Nabi ndiye mtu sahihi wa kushindana na mahasimu wao, Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns.

Ahmed Ally alia na kocha wa Dodoma Jiji

Baada ya Yanga SC kushinda mchezo wa Ligi kuu Soka Tanzania bara dhidi ya Dodoma Jiji kwa magoli 4-0, Meneja wa habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally kupitia mtandao wake wa Instagram amemtupia lawama Kocha wa Dodoma Jiji Mecky Mexime juu ya kauli zake. Ahmed Ally ameandika kuwa ''Dodoma Jiji jana kafungwa magoli mawili ya Uwongo, Moja la Offside na pili Penati ya uongo lakini Kocha wao hajalalamika kuonewa wala kudhulumiwa zaidi amesema AMESTAHILI KUFUNGWA. Rejea mechi ya Dodoma Jiji Vs Simba, baada ya sisi kufunga goli la Penati ya halali alitoa mapovu kulaumu Waamuzi yote ni kuaminisha watu kuwa tumemdhulumu na kutaka kutia dosari kazi nzuri inayofanywa na Simba Sports msimu huu. Nimeyasema haya ili Wana Simba tuone vita ni kubwa iliyombele yetu ni namna gani Wapinzani hawapendi kufungwa na sisi lakini wanafurahi kufungwa na wengine, ndio maana haishangazi kuona tunapata ushindi wa jasho na damu'' ''Wale wanaosema tunashinda lakini tunashikilia ...

CS SFaxien yaadhibiwa na CAF

Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limeitoza faini ya dola 50,000 (Zaidi ya milioni 120 za Kitanzania) timu ya CS Sfaxien ya Tunisia, pamoja na adhabu ya kucheza mechi mbili za nyumbani za kombe la shirikisho bila mashabiki. Mechi hizo zitakuwa ni dhidi ya Simba SC na FC Bravos ya Angola, adhabu hiyo imetolewa baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Simba uliochezwa December 15 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tanzania Prisons yaiteketeza Pamba Jiji

Timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya jioni ya leo imeichapa Pamba Jiji FC ya Mwanza bao 1-0 katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mchezo wa Ligi Kuu bara. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Tariq Abdallah Simba aliyefumua shuti la umbali wa mita 17 kumtungua kipa wa zamani wa Tanzania Prisons, Yona Geoffrey Amos dakika ya 31.

Mwaka 2024 ulikuwa mzuri kwenye soka

Na Prince Hoza BOXING Day inamalizika hii leo  baada ya jana kusherehekea X mass, nadhani mwaka 2024 unaelekea kwisha na siku kama ya leo yaani wiki ijayo itakuwa mwaka mpya. Jumatano ijayo ni sikukuu ya mwaka mpya wa 2025, yapo mambo mazuri ambayo tumeyaona mwaka huu na pia yapo mabaya tumeyaona, lakini mazuri ni mengi tena yakufurahisha. Kwenye mchezo wa soka ndio sehemu inayotazamwa na wengi ingawa pia kwenye mchezo wa masumbwi pia mazuri yamefanyika, bondia Hassan Mwakinyo naye ameingia kwenye rekodi ya waliofanya vizuri msimu huu. Mwakinyo alitetea mkanda wake wa WBO kwa upande wa Afrika, hayo ni mafanikio ya nchi kama nchi, lakini mwaka huu umekuwa mzuri kwa Tanzania kwenye upande wa soka na hasa timu zetu kufuzu kwenye michuano ya Afrika. YANGA KUFIKA ROBO FAINALI AFRIKA Mwaka 2024 klabu ya Yanga SC kwa mara yake ya kwanza ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya vilabu ya Ligi ya mabingwa Afrika, Yanga iliwagharimu miaka 25 kufika hatua hiyo baada ya kuvuka hatua ya maku...

Baleke atoboa siri kinachomweka benchi Yanga

Kupitia Ukurasa wake Tiktok Live, Jean Baleke alisema moja kati ya sababu kubwa ya kutofautiana na Uongozi wa Yanga ni suala la malipo ambayo yamechelewa kwa kipindi kirefu kidogo jambo ambalo lilimfanya ashindwe kutumika vizuri. “Nilipewa barua wiki iliyopita na kwangu naona ni uamuzi mzuri tu ambao klabu imefikia kwani sikuwa napata haki yangu kama ilivyotakiwa. Sijalipwa mshahara wangu miezi miwili, suala ambalo sio zuri kwa upande wangu, niko tayari sasa kwa changamoto mpya

Ditram Nchimbi atua Mbeya Kwanza

Klabu ya Mbeya Kwanza imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Yanga,Polisi,Njombe Mji na Mbeya City Ditram Adrian Nchimbi akitokea Biashara United. Nchimbi tayari amajiunga na Mbeya kwanza na yupo na kikosi hapa mkoani Arusha wakijianda na mchezo dhidi ya TMA Stars siku ya ijumaa.

Kibu Denis kurejea.......

Kibu Denis amesha anza safari ya kurejea Tanzania akitokea Marekani alipokuwa ameenda kwa ajili ya Matatizo ya kifamili. Kila kitu kiko sawa na Kibu anarejea nchini Sasa ili kuendelea na majukumu yake ndani ya Simba. Kibu alikosekana Katika Mchezo Kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar na Mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Yanga yaendeleza mauaji Ligi Kuu

Timu ya Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, jioni ya leo wameifunga timu ya Dodoma Jiji mabao 4-0 na kuendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya watani zake Simba. Ikicheza kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Yanga iliandikisha mabao yake kupitia kwa Clement Mzize aliyefunga mawili, Stephanie Aziz Ki na Prince Dube. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 36 ikizidiwa pointi moja tu na mtani wake Simba yenye pointi 37, Jumapili Yanga itaumana na Fountain Gate.

Namungo yaituliza Fountain Gate

Timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi mchana wa leo imewafunga mabao 2-1 timu ya Fountain Gate katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara mchezo wa Ligi Kuu bara. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na viungo Pius Charles Buswita dakika ya 10 na Geoffrey Julius Luzendaze dakika ya 78, wakati bao pekee la Fountain Gate limefungwa na winga Salum Kihimbwa dakika ya 30. Fountain Gate mwishoni mwa wiki hii itaumana na mabingwa watetezi Yanga SC katika kuwania pointi tatu muhimu

Kiungo MC Alger ashinda tuzo

Kiungo wa Klabu ya MC Algers Raia wa Ivory Coast Mohammed Zougrana (23) ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa kigeni ndani ya ligi kuu ya Algeria Maarufu kwa jina la ALBIR EBUSI kwa mwaka 2024, Tuzo hizo ziliandaliwa na Kusimamiwa na Kampuni ya ya DZ MATCH huku zikifahamika kwa jina la DZ Player of the Year 2024.

Ramovic amtosa straika mpya Yanga

Kocha Miguel Gamondi alileta straika mpya na kujifua na kikosi cha timu hiyo kambini, Avic Town, akisubiri kusaini mkataba wakati huu wa dirisha dogo, lakini alichokutana nacho kwa kocha wa sasa, Sead Ramovic, huenda kikamshangaza baada ya kuchomolewa kikosini humo. . Straika huyo aliyepigwa chini na Ramovic ni Fahad Bayo, raia wa Uganda aliyekuwa akijifua na kikosi cha sasa wakati akiangaliwa na Gamondi aliyetimuliwa mwezi uliopita. . Wakati Ramovic akitua Yanga alikutana na Bayo akiendelea na mazoezi, lakini kocha huyo amewaambia mabosi wa timu hiyo, anataka mtu wa maana katika eneo hilo zaidi ya Mganda huyo kwani kwa kiwango alichonacho hana tofauti kabisa na kila Clement Mzize, Prince Dube, Jean Baleke na Kennedy Musonda wanaotumika eneo hilo. . Ramovic amewaambia mabosi wa Yanga hataki historia anataka mashine zenye uwezo wa kukifanya kikosi chake kuwa bora. Inaelezwa Bayo aliyetokea MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech, uzito wa mwili wake ndiyo umemfanya kocha huyo kumkataa, kwani ame...

Serengeti Boys yafuzu AFCON U17

TIMU ya taifa ya vijana Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kukata tiketi ya AFCON U17 2025 nchini Morocco baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Sudan Kusini Uwanja wa Hamz, zamani Nakivubo Jijini Kampala katika Nusu Fainali ya kwanza ya michuano ya CECAFA U17.

Haji Manara afyata kwa jeshi la Magereza

Mwanachama maarufu wa Klabu ya Yanga SC, Haji Manara, ameomba radhi kwa mara nyingine kwa Jeshi la Magereza, Kamishna Mkuu, viongozi wa jeshi hilo na askari wake wote kufuatia sakata lililotokea siku ya mechi ya Yanga SC vs Tanzania Prisons katika Uwanja wa KMC. Manara ameweka wazi kwamba hana maneno yanayoweza kuzidi neno "Samahani", akisisitiza kuwa mazungumzo yake ya awali yalitokana na hisia za kishabiki. Pia amesisitiza heshima yake kubwa kwa Jeshi la Magereza na taasisi nyingine za dola nchini. "Heshima yangu kwa taasisi hii muhimu haiwezi kuwa na mbadala wa neno samahani," amesema kwa unyenyekevu mkubwa.

Simba yazidi kuunusa ubingwa

Lilikuwa ni bao la dakika ya 90 na ushei la mkwaju wa penalti wa Kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua aliyemchambua kipa Yacoub Suleiman wa JKT Tanzania baada ya beki Mohamed Bakari kumchezea rafu Shomari Kapombe kwenye boksi. Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukaa kileleni kwakufikisha pointi 37 na mwishoni mwa wiki hii itaumana na Singida Black Stars. Pia goli la Ahoua linamfanya afikishe mabao 7 kumsogelea kwa karibu kinara wa mabao Elvis Rupia mwenye mabao manane

Rupia azidi kutupia, Singida Black Stars ikiua

Timu ya Singida Black Stars leo mchana imeifunga KenGold mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Liti mjini Singida. Kwa matokeo Singida Black Stars imefikisha pointi 33 ikiendelea kushika nafasi ya nne nyuma ya Azam FC, KenGold walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Herbery Lukindo dakika ya 26. Lakini Josephat Arthur aliifungia Singida Black Stars bao kwanza dakika ya 46 na la kusawazisha, kabla ya Elvis Rupia dakika ya 56 kufunga bao la ushindi. Kipigo hicho kwa KenGold kimeifanya timu hiyo izidi kuchungulia kaburi la kushuka daraja, Singida sasa itaumana na Simba mwishoni mwa wiki

Morrison atua KenGold

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga, Bernard Morrison raia wa Ghana amekamilisha usajili wa kujiunga na timu ya KenGold ya Chunya mkoani Mbeya. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ni kwamba Morrison amesajili kwa kandarasi ya mwaka mmoja, KenGold iko kwenye tanuru la kutelemka daraja.

Jeshi la Magereza latoa onyo kwa wanaolibeza

Uongozi wa Jeshi la Magereza limetoa onyo na kuwataka kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza au kudharau Mamlaka yake. Kauli hiyo imetolewa na Msemani wa Jeshi la Magereza baada ya kipande cha video kilichosambaa mtandaoni kikimuonesha, Ndugu Haji Manara kukataa kwa dharau na kuanza kutoa maneno yasiyo ya kiungwana baada ya kuombwa kutoa gari lake mbele lililozuia gari la Jeshi la Magereza.