TAIFA la Tanzania bado lipo kwenye mikono salama usiku huu baada ya Bondia Mtanzania Mchanja Yohana kutembeza kichapo usiku wa jana kwa kumchapa makonde ya kutosha bondia kutoka Philipino Miel Fajardo na kushinda kwa pointi 116 kwa 111 za majaji wote watatu.
Pambano hilo la raundi 12 kwenye pambano la Knock out ya Mama ndani ya ukumbi wa Super Dome hapa Masaki na kufanikiwa kushinda mkanda wa World Boxing Organization Global flyweight championship (WBO Global).
Kwa ushindi huo wa pointi, Mchanja anaondoka na kitita cha KnockoutYaMama cha Sh milioni tano (5 Milioni).