Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed
Suleiman Moroco amemuondoa kwenye timu Mchezaji Abdulaziz
Makame "Bui" wa Geita Gold FC kwa makosa ya utovu wa nidhamu
pamoja na kutokufika Kambini kwa wakati, huku akiwa amesharuhusiwa
na timu yake kwa muda mrefu.
Moroco amewaongeza kwenye timu, Abubakar Nizal kutoka Azam FC U20 na Abdulnasir Mohamed Abdallah 'Casemiro' Mlandege FC